HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 31, 2024

TAASISI YA ELIMIKA WIKIENDI ORGANIZATIION WAZINDUA KLABU YA AFYA YA AKILI

Shirika lisilo la kiserikali la Elimika Wikiendi Organization linaloendesha jukwaa la elimu katika mtandao wa Twitter maarifu kama #ElimikaWikiendi, leo 31 Mei 2024 limezindua Klabu ya afya akili shule ya sekondari Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha maadhimisho ya mwezi wa kukuza uelewa kuhusu masuala ya afya ya akili duniani.

Lengo mahsusi la ufunguzi wa klabu hiyo ni kuwajengea vijana wadogo uwezo wa kukabiliana na changamoto za afya ya akili katika mazingira ya shuleni na nyumbani kwa ustawi bora na ustahimilivu.

klabu hii inalenga pia kukuza uelewa kuhusu masuala ya afya ya akili na kutoa msaada wa haraka inapobidi ili kupafanya shuleni na nyumbani pawe sehemu salama kwa watoto kujifunza, kukua na kustawi kwa ufaulu na maendeleo bora ya kitaaluma.

Klabu hiyo iliyozinduliwa mapema leo ni moja ya programu muhimu ndani ya mradi wa MIND YOUR MIND ambapo jumla ya wanafunzi 30 wa kike na wa kiume watanufaika na mafunzo, semina, warsha, midahalo baina yao wenyewe, na ikibidi kuunganishwa na washauri na wataalamu mbalimbali wa masuala ya afya ya akili kwa msaada zaidi.

Katika ufunguzi wa klabu hiyo, Ndugu Jokate Mwegelo ambaye pia ndio mlezi wa klabu hiyo aliweza kuzungumza na watoto kwa njia ya simu akieleza umuhimu wa mazingira salama ya shule katika kujifunza na katika mafanikio yao ya kitaaluma.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad