HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 15, 2024

Rais Dkt. Hussein Mwinyi atembelea Banda la Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC)

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi  ametembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania na kupata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Bw.Aristid Kanje kwenye Kongamano la Sita la Afrika Mashariki la wadau wa masuala ya Usafiri wa Anga.

Kongamano hilo la sita linafanyika visiwani Zanzibar kuanzia 15-16 Mei 2024 chini ya Udhamini wa TCAA ikishirikiana na CASSOA.

CATC moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi  akipata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Bw.Aristid Kanje alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania na kwenye Kongamano la Sita la Afrika Mashariki la wadau wa masuala ya Usafiri wa Anga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Aristid Kanje alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania na kwenye Kongamano la Sita la Afrika Mashariki la wadau wa masuala ya Usafiri wa Anga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad