HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 26, 2024

MRAMBA AONYA WANAOTEMBEA NA MAJINA YA WAGOMBEA MIFUKONI

 Na Khadija Kalili Michuzi Tv
KATIBU wa Siasa,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),David Mramba ametoa onyo kali kwa baadhi ya wanachama wake kwa watu walioanza kampeni kabla ya wakati wa uchaguzi huku baadhi ya wanachama wake wakitembea na majina ya wagombea mifukoni mwao kua watachukuliwa hatua kali za kwenda kinyume na maadili.

"Nasema ni marufuku kwa kundi ama Taasisi yoyote kujihusisha na kampeni hizi chafu na isivyo halali na ndiyo maana katika baadhi ya maeneo kunafanyika fujo kwa Wabunge , Madiwani na Venyeviti wa Eerikali za Mitaa na Vitongoji nasema ukibainika na nikajiridhisha tutakuchukulia hatua kali za nidhamu" amesema Mramba.

Mramba amesema hayo Mei 25 katika mafunzo ya siku moja kwa wanachama wa CCM Mkoa wa Pwani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kibaha.

Mbali ya kukemea hilo pia amewageukia vikundi na taasisi ambazo zinajiendesha katika masuala ya siasa ndani ya Mkoa wa Pwani ambao hawajasajiliwa na kuwataka kuhakikisha wamepata usajili ifikapo Juni30 mwaka huu ili waweze kutambulika katika utendaji wa kazi za Chama Cha Mapinduzi (CCM)ndani ya Mkoa.

"Nawasisitiza Taasisi zote ndani ya Mkoa wa Pwani hakikisheni mnapata usajili halali ili muweze kutambulika rasmi na kufanya kazi zenu kwa uhuru huku mkizingatia miiko ya Chama na Serikali"
amesema Mramba.

Aidha amewaambia viongozi wa Taasisi hizo kuwa endapo watakutana na vikwazo katika kupata usajili huo wasisite kwenda kumuona ofisini kwake milango iko wazi muda wote ili aweze kuwasaidia kwa sababu wote wanajenga nyumba moja hivyo hakuna haja ya kugombea fito.

Aidha amewaeleza Viongozi wa Taasisi hizo kuzingatia kuwa na malengo ya kunufaisha taifa na si kujinufaisha binafsi huku akiwaasa kutotumia hizo taasis zao kama kichaka cha kuhifadhi maovu bali wawe sehemu sahihi ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu mambo yote mazuri yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na seeikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Tumieni Taasisi zenu kwa kutoka elimu yenye manufaa kwa jamii hasa umuhimu wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika baadaye mawaka huu na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo nasema kwa sisi wa Mkoa wa Pwani jina na fomu ya kiti cha urais ni moja tu ya mama Jemedari wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan" amesema Mramba.

Aidha katika mafunzo hayo walikuwepo watoa mada mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad