HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 26, 2024

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UAPISHO WA RAIS WA COMORO

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 26 Mei 2024 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Sherehe za Uapisho wa Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Malouzini uliopo Moroni nchini Comoro.

Katika hafla hiyo Makamu wa Rais ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohamed, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka Barani Afrika na Nje ya Bara la Afrika.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiwasili katika Uwanja wa Michezo wa Malouzini uliopo Moroni nchini Comoro kushiriki Uapisho wa Rais Mteule wa Comoro Mhe. Azali Assoumani tarehe 26 Mei 2024.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wakiungana na Viongozi kutoka Mataifa mbalimbali pamoja na Wananchi wa Comoro wakati wa Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Comoro Mhe. Azali Assoumani zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Malouzini uliopo Moroni tarehe 26 Mei 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimpongeza Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani mara baada ya kuapishwa katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Malouzini uliopo Moroni nchini Comoro tarehe 26 Mei 2024

Rais wa Comoro Mhe. Azali Assoumani akiapishwa katika sherehe zilizofanyika katika katika Uwanja wa Michezo wa Malouzini uliopo Moroni tarehe 26 Mei 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad