HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 9, 2024

KAMPUNI YA AIRTEL YAHITIMISHA KAMPENI YA UPIGE MWINGI MPAKA AFCON

Meneja Mahusiano kutoka Airtel, Jackson Mbando akizungumza na Mshindi wa  droo ya mwisho ya kampeni ya upige mwingi mpaka Afcon Kila mmoja ni Mshindi  jijini Dar es Salaam leo Mei 09, 2024. 

Meneja Mahusiano kutoka Airtel, Jackson Mbando akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 09, 2024 wakati akiendesha droo ya mwisho ya kampeni ya upige mwingi mpaka Afcon Kila mmoja ni Mshindi.Kampeni hiyo ilianza mwezi januari mwaka huu na imehitimishwa hii leo ikiwa imetimiza siku 90 tangu ianze.

Baadhi ya washindi wa Simu wakiwa na simu zao waliofika katika ofisi za Airtel Dar es Salaam kwaajili ya kuchukua zawadi zao.
Meneja Mahusiano kutoka Airtel, Jackson Mbando  akiwa na washindi wa simu leo Mei 09, 2024 jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Airtel Tanzania leo Mei 09,2024 imehitimisha kampeni ya upige mwingi mpaka Afcon Kila mmoja ni Mshindi kwa kuwapa zawadi washindi wa simu pamoja na kuchezesha mchezo wa bahati nasibu wa mwisho.


Mchezo wa mwisho wakati wa kufunga kampeni hiyo watu wawili wamejinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na Televisheni ya Smati pamoja na Pikipiki.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akiendesha droo ya mwisho ya kampeni hiyo, Meneja Mahusiano kutoka Airtel, Jackson Mbando amesema kampeni hiyo ilianza mwezi januari mwaka huu na imehitimishwa hii leo ikiwa imetimiza siku 90 tangu ianze.


Ameeleza kuwa kampeni hiyo imekuwa na zawadi mbalimbali pamoja na baadhi ya washindi kwenda nchini Ivory Coast kushuhudia michuano ya Afcon.


Aidha Mbando Ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kutumia huduma za Airtel ili wajishindie zawadi pale zinapojitokeza kampeni kama hiyo iliyomalizika leo.


Kwaupande wake Mkazi wa Magomeni Dar es Salaam, Sophia Mnywaki mmoja wa washindi ambaye amejishindia simu ya mkononi, alishukuru kampuni hiyo ya simu kwa zawadi, huku akitoa rai kwa Watanzania kutumia huduma zaidi wajishindie safari ya kwenda nchini Ivory Coast.


Kwa upande wa washindi wa Simu waliofika leo kwaajili ya kuzichukua zawadi hizo za simu walizojishindia wamewashukuru kampuni hiyo kwa kuendesha kampeni zenye ukweli na uwazi kwa kuwa wanatumia namba 100 kwaajili ya kuwapigia washindi wa michezo ya kubahatisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad