HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 1, 2024

Barrick yaendeleza rekodi ya ushindi wa juu wa jumla tuzo za Wiki ya Usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA)

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mary Maganga (wa pili kulia) wakikabidhi tuzo ya ushindi wa Jumla kwa wafanyakazi wa Barrick (kutoka kushoto) ni Hassan Kallegeya Safety Coordinator (Bulyanhulu) na kulia ni Aristides Medard (Specialist Occupational Hygiene, Katika hafla iliyofanyika jijini Arusha. Mbali na ushindi wa Jumla Barrick imeshinda tuzo nyingine 4
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nicolaus Mkapa, akimkabidhi tuzo kwa ushindi wa kwanza katika sekta ya madini kwa Mtaalamu wa masuala ya Usalama wa Barrick –Specialist Occupational Hygiene, Aristides Medard katika hafla ya kukabidhi tuzo iliyofanyika jijini Arusha. Wengine pichani ni Wafanyakazi wa Barrick. Mbali na ushindi wa Jumla Barrick imeshinda tuzo nyingine 4.
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo ambazo kampuni imejishindia.

Na Mwandishi Wetu.

Barrick Tanzania imenyakua tuzo tano katika hafla ya utoaji wa tuzo za Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ya 2024 iliyofanyika jijini Arusha ambapo Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, umeshinda tuzo kubwa ya mshindi wa juu wa Jumla katika Tuzo ya Afya na Usalama (OHS) 2024.

Mbali na ushindi huo mkubwa, Bulyanhulu, pia ilinyakua tuzo za Utawala Bora ofisini, usaidizi wa kiofisi na shughuli za ukuzaji biashara , na mshindi Bora wa Ubunifu kwenye maonyesho ya OSHA ya mwaka huu kwenye sekta ya madini.

Kwa upande wake, Barrick North Mara ilishinda tuzo ya juu katika Kuwajali Zaidi Wafanyakazi wenye Mahitaji Maalum.

Maonyesho ya OSHA mwaka huu yalifanyika katika viwanja vya General Tyre jijini Arusha, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwaka huu ambapo aliwakilishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Patrobas Katambi.

Barrick Tanzania imeshinda tuzo za 2024 kutokana na mafanikio ya 2023 ya kampuni ambapo ilishinda tuzo ya jumla ikiwemo tuzo za uandaaji Ripoti Bora ya Tathmini ya Hatari katika uchimbaji madini na mshindi Bora wa tuzo ya Usalama na afya (OHS) katika sekta ya madini.

Tuzo nyingine ilizoshinda zilikuwa ni Kujali zaidi Wafanyakazi wenye Mahitaji Maalum na utekelezaji sera bora ya Usalama mahali pa kazi (OHS), mshindi wa pili kwa washindi wa jumla wa sekta ya Madini, utekelezaji Mpango Kazi Bora wa Usalama na Afya mahali pa kazi.

Usalama ni sehemu muhimu ya DNA ya Barrick. Kampuni ina mpango maalum kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wake na wakandarasi, kuhakikisha kwamba kila mtu anarudi nyumbani akiwa na afya njema na salama. Juu ya yote hayo katika Barrick kila mtu amejitolea kufanya a kuhakikisha hakuna matukuo ya ajali katika sehemu yake anapofanyia kazi.

Katika maonesho ya mwaka huu Barrick pia ilifiikisha elimu ya afya na usalama kwa wananchi waliotembelea kwenye banda lake kwenye maonesho haya sambamba na kushiriki zoezi la kupanda miti katika kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya maonesho ya athari za mabadiliko ya tabia nchi katika usalama na afya kazini:sajili eneo lako la kazi OSHA katika harakati za kupunguza athari hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad