HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 31, 2024

BALOZI NCHIMBI AZUNGUMZA NA WANANCHI KATA YA ITAJE, SINGIDA KASKAZINI

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akizungumza na Wananchi wa Kata ya Itaje, Jimbo la Singida Kaskazini, wakati akiwa njiani kuelekea Manyara ikiwa ni katika muendelezo wa ziara yake ya mikoa mitano.

Ziara ya Dkt Nchimbi inalenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ipo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020/2024 pamoja na kuzungumza na makundi mbalimbali ya Kijamii.

Kupitia ziara hiyo Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Mambo ya Siasa na uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad