HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 6, 2024

AIRTEL TANZANIA YATOA GAWIO LA FAIDA YA BILIONI 3.9 KWA WATEJA WANAOTUMIA HUDUMA ZA AIRTEL MONEY

 

AIRTEL MONEY TANZANIA imetangaza kutoa kiasi cha bilioni 3,956,681,813 TZS kama Gawio la Faida la Airtel Money zitakazogawanywa kwa Wateja na Mawakala wa Airtel Money nchi nzima ambao wamekuwa wakitumia huduma za Airtel Money kati ya Julai hadi Desemba 2023.

Utoaji wa Gawio la Faida ya Airtel Money ni uthibitisho wa kuendela kufanikiwa kwa mikakati ya Airtel money katika kuboresha huduma za kifedha kupitia Airtel Money ili kutoa huduma bora, zenye ubunifu na nafuu kwa wateja. Gawio la Faida la Airtel Money linagawanywa kwa wateja na Mawakala kuanzia sasa.

Gawio la Faida ya Airtel Money hutolewa kwa wateja na mawakala wa Airtel Money kila robo ya mwaka kulingana kiasi na alichoweka kwenye akaunti yake ya Airtel Money. Kiasi cha gawio anachopata kitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya Airtel Money.

Wateja wa Airtel Money wataweza kutumia kiasi cha gawio la faida ya Airtel Money wapendavyo ikiwemo kujinunulia muda wa maongezi, kutoa kwa wakala au kulipia bili kama vile DAWASCO, LUKU, na nyinginezo.

Airtel Money ilianza kugawa gawio la faida tangu mwaka 2015 ambapo hadi leo imeshagawa jumla ya bilioni 52 kwa wateja na mawakala wake nchini nzima.

"Airtel Money Tanzania tutaendea kutekeleza dhamira yetu ya kutoa huduma nafuu na kuleta mifumo bora ya kupanua miundombinu ya huduma zetu ili kuendelea kusambaa na kutoa huduma vijijini na mjini,” alisema Andrew Rugamba, Mkurugenzi wa Airtel Money.

Aliongeza "Airtel Money tutaendelea kupanua zaidi mtandao wa mawakala ili kuhakikisha huduma zote za Airtel Money zinapatikana kwa urahisi kwa wananchi walio wengi."

Airtel inajivunia miundombinu yake ya usambazaji ya Airtel Money nchini, ambapo ina zaidi ya Airtel Money Branch 4,000 pamoja na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 250,000 nchi nzima. Vilevile, Airtel Tanzania imejiunganisha na mifumo ya malipo kielektroniki, ikiwemo ya serikali ili kuwawezesha wateja kufanya malipo mbalimbali ya serikali wakiwa popote.

Airtel Money pia imeunganishwa na zaidi ya benki 40 nchini, hivyo kuwawezesha wateja wa Airtel Money kufanya miamala ya kifedha kutoka kwenye akaunti zao za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money kwa urahisi, huku wakifurahia kutuma pesa kwa wateja wa Airtel bila gharama yoyote.

Airtel Money Tanzania inaendelea kujizatiti katika kuboresha huduma za kifedha kupitia simu kwa wateja wake na itandelea kubuni huduma mbambalia kutokana na mahitaji ya wateja wake na watanzania kwa ujumla ili kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha kidijitali na kuondoa changamoto ya kutofikiwa na huduma za kifedha popote nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad