HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 19, 2024

Waongoza ndege kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCAA) wahitimu katika cha CATC

 


Wahitimu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC), kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCAA) wamekumbushwa kwamba kusoma hakuishii darasani pekee, mengine wataendelea kujifunza maofisini mwao wakati wanafanya kazi husika kwa vitendo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA Bi Flora Alphonce aliyekuwa mgeni rasmi Aprili 19, 2024 wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance). Na kuongeza kuwa anaishukuru UCAA kwa kuendelea kukiamini chuo cha CATC na kuendelea kuleta watalaam wake kwa mafunzo.

Bi Flora aliwafahamisha wahitimu hao kwamba chuo cha CATC ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo kitakuwa na majengo na vifaa vya kisasa ambavyovitaongeza tija na kuleta utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza hapa na pale kufuatia Serikali ya Tanzania kutenga Shilingi bilioni 78 kwa ajili ya mradi huo.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha CATC Bw.Aristid Kanje alisema amefurahishwa na kuwapongeza wahitimu hao wote kwa kumaliza kozi zao kwa ufaulu wa juu. Na kuongeza kuwa ni vugumu kumlazimisha mtu kupata maarifa, kwani maarifa yanapatikana kwa kuwa na hamu ya kuyapokea.

Wahitimu hao watano kutoka UCAA walifanya kozi mbili kwa muda wa wiki 12, awali kabla ya mahali wahitimu hao walipatiwa semina juu ya umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao kutoka kwa Daktari Concethar Mushi.

Akitoa salamu za shukran kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe aliishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake kwamba kwa kuhitimu kwao watu wana matarajio makubwa kwao hasa ya kutokufanya makosa.
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege TCAA, Flora Alphonce akizungumza na wahitimu wa  mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akizungumza jambo pamoja kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege, Flora Alphonce akiwakabidhi vyeti pamoja na zawadi kwa  wahitimu wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akizungumza na wahitimu wa  
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC). 
Dkt. Concethar Mushi akitoa mafunzo kuhusu umuhimu wa masuala ya kiafya na namna yanavyoweza kuathiri waongoza ndege katika majukumu yao wakati wa mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Kiongozi wa darasa hilo kwa niaba ya wenzake Bw. Erasmus Muhairwe akishukuru CATC kwa ushirikiano iliyowapatia kwa muda wote wa kozi zao na kuwakumbusha wahitimu wenzake wakati wa 
mahafali ya kozi za mbili za Uongozaji ndege(Area Control Procedural& Area Control Survellance) yaliyofanyika katika chuo Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) 
Wahitimu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Uganda (UCAA) wakiwa kwenye mahafali hayo


Picha ya Pamoja

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad