HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 10, 2024

USIKU WA LIGI YA MABINGWA ULAYA HAKUPOI HAKUBOI LEO

 

LIGI ya mabingwa ulaya itaendelea tena leo hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo itaenda kupigwa michezo miwili mikali katika viwanja viwili vikubwa barani ulaya.

Atletico akiwa kwenye fomu nzuri kabisa watakua nyumbani kulikaribisha jeshi la njano na nyeusi kutoka kule nchini Ujerumani, Huku PSG vinara wa ligi kuu ya Ufaransa kuwaalika klabu ya Fc Barcelona kutoka nchini Hispania.

Usiku wa leo klabu ya Paris Saint German itakua nyumbani katika dimba la Parc De Princes kuwakaribisha klabu ya Barcelona katika mchezo wa robo fainali wa ligi ya mabingwa ulaya mkondo wa kwanza.

Paris Saint German mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa watakua kwenye mkakati wa kupambana kulitafuta taji lao la ulaya kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo, Lakini wakati huohuo wanakutana na Barcelona ambayo ina uzoefu mkubwa kwenye michuano hiyo hivo mchezo huu unatarajiwa kua mkali kwelikweli.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Kipute kingine kitapigwa pale katika dimba la Wanda Metropolitano ambapo klabu ya Atletico de Madrid itaikaribisha klabu ya Borussia Dortmund kutoka kule nchini Ujerumani, Huku mchezo huo ukitarajiwa kua wenye ushindani mkubwa baina ya vilabu hivyo.

Atletico Madrid wamekua kwenye ubora mkubwa wakifanikiwa kumtoa mwanafainali wa michuano iliyopita klabu ya Inter Milan ya nchini Italia huku wakipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo, Lakini Dortmund ni moja ya vilabu ambavyo vimekua vikifanya vizuri linapokuja michuano ya ulaya.

Michezo yote ya leo inapatikana pale Meridianbet na imepewa ODDS KUBWA ambazo zinaweza kukufanya ukaibuka na mkwanja wa kutosha, cha kufanya ni wewe kutengeneza mkeka wako kupitia michezo hii ya kukata na shoka uweze kupiga mkwanja.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad