Na Mwandishi wetu.
Mashabiki
wa soka, tenisi, UFC, Kriketi, baseball na michezo mingine sawa
wanaweza kushinda tiketi ya kwenda Dubai kwa kubashiri na kampuni ya
Parimatch Tanzania.
Pia kampuni hiyo imeingia mkataba na
muigizaji nyota, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa kuwa
balozi wa chapa yao, “Brand Ambassodor”.
Mbali
ya Zaylissa, pia mchekeshaji maarufu nchini, Vincent Njau “Kiredio”
naye ametangazwa kuwa balozi chapa wa Parimatch wakiungana na meneja wa
habari wa zamani wa Yanga, Haji Manara.
Kwa mujibu wa Mkuu wa
Masoko wa Parimatch, Levis Paul, jumla ya mashabiki nane (8) watashinda
tiketi hiyo kupitia promosheni hiyo ya Twenzetu Dubai na Parimatch
ambayo imezinduliwa jana kwenye hotel ya Serena.
Paul alisema
kuwa kutakuwa na droo ya kutangaza washindi kila Alhamis na dhumuni
kubwa la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwawezesha wateja wao kuendelea
kufurahia ushindi.
Alisema kuwa mbali ya zawadi ya kwenda Dubai,
pia kutakuwa na bonasi ya Sh5,000 kwa yeyote atakayejisajili na
Parimatch na kucheza mchezo pendwa wa Aviator.
“Promosheni hiii
ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wenye akaunti na hata
wateja wapya watakaojiunga katika kipindi kipindi hiki. Lengo kampeni
hii ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kucheza na kufurahia burudani
kabambe za falme za kiarabu huko Dubai.
Kuanzia Aprili 29 mpaka
Juni 30, mteja wa Parimatch akifanya bashiri kwenye mchezo wa Aviator
ndani ya Parimatch Casino kupitia tovuti yetu www.parimatch.co.tz au App
yetu na kadri unavyoweka beti zaidi ndivyo unajiongezea nafasi ya
kujishindia tiketi ya kwenda Dubai au kujishindia bonasi ya Sh5,000 kila
siku”, alisema Levis.
Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa
michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya
ukaribisho ya asilimia 125 hadi kufikia Sh 1,000,000 kwa wateja wapya
wanaojiunga nao.
Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania
tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds
kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya
virtual.
Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya
matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball
na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.
Wakati huo huo,
Zaylissa amesema amefarijika sana kuwa balozi wa Parimatch na atafanya
kazi hiyo kwa bidii zote ili kuleta tija katika kampuni hiyo.“Nawaomba
mashabiki zangu wajiunge na Parimatch , kubashiri na kushinda ili kupata
nafasi kwenda Dubai,” alisema Zaylissa.Muigizaji
maarufu, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa (kushoto)
akionyesha mkataba aliosaini na kampuni ya michezo ya kubashiri ya
Parimatch kuwa balozi chapa (Brand Ambassodor). Mbali ya kusainiwa kwa
mkataba huo, pia Kampuni ya Parimatch ilizindua promosheni ya Twenzetu
Dubai ambayo itapeleka washindi nane watakaobashiri kuitia mchezo wao wa
Aviator.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Eric
Gelard (kushoto) akisaini mkataba na muingizaji nyota nchini, Zainab
Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa kuwa balozi chapa wa kampuni
hiyo. Utiaji saini huo ulifanyika sambamba na uzinduzi wa promosheni ya
Twenzetu Dubai ambayo washindi nane watapata fursa ya kutembelea nchi
hiyo baada ya kubashiri kupitia aviator.
Mkuu
wa Masoko wa kamouni ya kubashiri ya Parimatch, Levis Paul akizungumza
wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Twenzetu Dubai ambayo jumla ya
mashabiki nane (8) wa michezo watakaoshinda watatembelea nchi hiyo na
kukaa kwa muda wa siku nne.
Muigizaji
maarufu, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa (kushoto)
akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Twenzetu Dubai ya
kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch. Zaylissa ni Balozi Chapa
wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Parimatch Tanzania, Levis
Paul.
No comments:
Post a Comment