HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 8, 2024

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA DUA YA KUMUOMBEA RAIS SAMIA

Picha ya pamoja katika Iftari katika Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma ikiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (Mwenye ushungi wa rangi ya orange).
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akila chakula na watoto katika Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akikabidhi zawadi kwa ajili ya sikukuu ya Eid katika Kituo cha kulea watoto yatima na wenye mahitiji maalum cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akihudumia chakula wakati wa Iftari iliyofanyika katika Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma.


Na. Mwandishi wetu- Dodoma
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameongoza dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan pia ameungana na Viongozi wa Dini na wananchi kupata Iftar ya pamoja.

Akizungumza mara baada ya dua hiyo iliyofanyika jana Aprili 7, 2024 katika Kituo cha kulea watoto yatima cha Rahmaan kilichopo Chang’ombe Jijini Dodoma, Mhe. Nderiananga amesema kuwa uamuzi huo wa kufanya dua ya kumuombea Rais Samia ni kwa sababu ya mambo mengi aliyoyafanya katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, maji, afya na miundombinu.

Aidha, Mhe. Nderiananga amewasihi Watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu ili Taifa liendelee kuwa katika hali ya amani na usalama.

“Tumeamua kufanya dua hii maalum ya kumuombea Mhe. Rais na viongozi wetu wa Serikali pamoja na wazazi wangu”. Amesema Mhe. Nderiananga.

Ameongeza “Tunashukuru sana uongozi wa kituo hiki kwa dua nzuri kwa watoto na malezi mazuri ya hawa watoto wetu naamini wamejisikia vizuri na kufurahi tulivyowatembelea leo”.

Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amewashauri watoto hao wasome kwa bidii ili kutimiza ndoto zao huku akiwataka kuepuka kujiingiza katika makundi mabaya yatakayosababisha kutotimiza malengo yao.

Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi. Rukia Hamis Abdallah ameeleza kwamba kituo hicho kinachohudumia watoto 120 kilianzishwa kwa lengo la kujiendeleza kielimu katika maadili mema ya dini, kusaidia watoto pamoja na watu wanaoishi katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad