HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 1, 2024

MBEYA; Jeshi la Polisi Linamtafuta mtu au Watu Waliohusika Katika Tukio la Mauaji

 

JESHI  la Polisi Mkoa wa Mbeya linamtafuta mtu au watu waliohusika katika tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Heriety Lupembe [37] na Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Isenyela Ivon Tatizo [15] wote wakazi wa Kijiji cha Kiwanja Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea Machi 31, 2024 majira ya saa 2:30 usiku wakati marehemu akiwa nyumbani kwake sebuleni na watoto wawili Ivon Tatizo na Haris Barnaba Mtweve [06] Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Ken Gold aliyejeruhiwa kwa kupigwa kitu butu kichwani.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, mtu huyo aliwavamia marehemu na kuanza kuwashambulia na baada ya kufanya hivyo alifunga milango kwa nje na kuondoka na funguo. Chanzo cha tukio hili bado kinachunguzwa. Majeruhi mtoto Haris Mtweve anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni Pamoja na msako dhidi ya mtu au watu waliohusika. Aidha, linatoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa za mtu au watu waliohusika katika tukio hili kutoa taarifa ili wakamatwe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad