HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 2, 2024

MAGESA ACHIMBA MSINGI WA BWENI NA WANANCHI LUTOZO

 



Na Nasra Ismail, Geita
MBUNGE wa jambo la Busanda Tumaini Magesa ameahidi ndanibya mwezi mmoja na nusu kukamilisha ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Lutozo iliyopo katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro mkoani Geita.

Ameyasema hayo asubuh ya Leo aliposhiriki katika kuchimba msingi wa bweni hilo ambalo linatakiwa kutumika katika msimu mpya wa masoma ya kidato cha tano mwaka huu.

Shule ya Sekondari Lutozo imekuwa ikifanyq vizuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa takribani miaka 5 hivyo kufanya shule hiyo kupata hadhi ya kuwa na masomo ya kidato cha tano na cha sita.

Magesa pia alipata wasaa wa kusikiliza kero za wananchi ambapo kero kubwa ni utiririshwaji wa maji yenye kemikali kutoka kwenye maplanti kwenda kwenye mito ya maji ya matumizi ya binafamu mbapo mbunge Magesa aliahidi kuita wataalam kupata majibu juu ya usalama wa maji na pia kuongea na wamiliki ili waweze kuzuia utiririshwaji huo.

Nae Diwani wa kata ya Katoro Kigongo Benedict Sweya alimshukuru na kumpongeza mbunge huyo kwa kutoa shilingi milioni 5 kutoka kwenye mfuko wa jambo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bweni hilo.

"Mheshimiwa Mbunge tumeshiriki hapa na mimi matajio yangu kwamba mwaka huu tunaenda kupokea watoto wa kidato cha tano nina imani umewapigia wadau na wamekubali kushiriki kwakuwa wana imani kubwa na wewe na imani ndani ya mienzi hiyo ujenzi utakuwa umekamilika" alisema Kigongo.

Aidha alimuomba mbunge kuwasaidia kupata kisima katika shule hiyo kwani imekuwa changamoto kubwa hata ikiwa shule inaelekea kupata wanafunzi wa bweni ambao wanahitaji maji ya mara kwa mara

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad