HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 6, 2024

Halotel Yatia mkono Uongozi wa mtaa wa Bwawani kupitia ufadhili wa Tukio la Iftar.

 Kampuni kubwa ya mawasiliano Halotel, inayoendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa jamii, imejitolea kudhamini tukio la Iftar kwa uongozi wa mtaa wa Bwawani na jamii ya watu wa Makumbusho kwa ujumla.

Halotel akiwa ni mtoa huduma wa mawasiliano Tanzania, akitoa huduma mbalimbali za mawasiliano na akiendelea kukidhi mahitaji ya wateja wao. Kwa kuzingatia utoaji huduma bora na uaminifu Halotel inaendelea kutoa huduma bora na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya mawasiliano na jamii kiujumla.

Tukio hili la Iftar linalenga kuileta pamoja jamii katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Halotel inaamini katika umoja na mshikamano kama kauli mbiu ya kampuni inavosema ‘Pamoja kwa Ubora’ na tumeona ni muhimu kusaidia juhudi za serikali kuleta watu pamoja na leo tupo tena Makumbusho katika kukuza uhusiano mzuri wa jamii zinazotuzunguka.

Kwa niaba ya Uongozi wa uongozi wa Bwawani, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani Ndugu Ismail Mwenda alishukuru kampuni ya Halotel Tanzania kuonesha nia ya kuunganisha watu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. “Hii ni chachu katika jamii kampuni inapoamua kuunganisha watu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, inaonesha upendo na mshikamano kati ya watu wa Makumbusho na jamii kiujumla” aliendelea kusema Ndugu Israel Mwenda.

“Katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, Halotel kwa ushirikiano na Serikali tunajivunia kuandaa iftar kwa ajili ya Jamii yetu” Aliongea Naibu Mkurugenzi wa Fedha Halotel “Hii ni ishara ya Umoja wetu, mshikamano na undugu unaotuunganisha sote. Ni wakati wa kushiriki, kusadiana na kuimarisha mahusiano yetu katika jamii” alimalizia Ndugu Najib Ferej.

Kupitia udhamini huu, tunawawezesha uongozi wa mtaa wa Makumbusho kufanya tukio la Iftar kuwa la kipekee na la kumbukumbu kwa wakazi wa Makumbusho na wafanyabiashara wadogowadogo wanaozunguka eneo hili. Halotel inatambua umuhimu wa kujenga jumuiya zenye upendo na tunaamini kuwa tukio hili litakuwa fursa nzuri ya kuimarisha mahusiano ya kijamii na kukuza utamaduni.

Halotel haitoishia hapa katika kuweka mkono katika jamii, tutaendelea kuweka nguvu katika kukuza umoja na mshikamano katika jamii yetu vivo hivyo Halotel itaendelea kuboresha huduma zake ambazo zinarahisisha mawasiliano mijini na kijijini.
Halotel Tanzania yashirikiana na Uongozi wa mtaa wa Bwawani katika kufturisha Mtaa wa Makumbusho. Tukio hili la Iftar limelenga kuongeza upendo na Ushirikiano katika Jamii katika kipindi hiki cha Ramadhan.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad