HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 25, 2024

WADAU WA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MUSTAKABALI WA TANZANIA KUJIUNGA NA SOKO LA PAMOJA AFRIKA


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imekutana na wadau wa sekta hiyo kujadili mustakabali wa Soko la Pamoja la Usafiri wa Anga na kupata maoni yao na kuona namna bora ya Tanzania kujiunga na soko hilo kwa kuendelea kulinda ustawi wa soko la ndani.

Akifungua mkutano huo wa siku nne unaofanyika katika ofisi za TCAA Banana - Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari amesema huu ni mkutano muhimu sana kwani maoni ya kila mdau yanahitajika katika kuimarisha sekta ya Usafiri wa Anga hapa nchini lakini pia kuingia katika soko huru la Afrika tukiwa tunazungumza kwa lugha moja.

Sambamba na hilo wadau wa mkutano huu watajadili mabadiliko na maboresho ya sheria za Usafiri wa Anga nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa sekta ya Anga ili kujadili mustakabali wa Soko la Pamoja la Usafiri wa Anga na kupata maoni yao na kuona namna bora ya Tanzania kujiunga na soko hilo kwa kuendelea kulinda ustawi wa soko la ndani.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akiwasilisha mada kwa wadau wa sekta ya Anga waliofika kwenye mkutano huo.
Mwanasheria Mwandamizi TCAA Massa Mumburi akiwasilisha mada kwa wadau wa sekta ya anga waliofika ili kujadili mustakabali wa Soko la Pamoja la Usafiri wa Anga na kupata maoni yao na kuona namna bora ya Tanzania kujiunga na soko hilo kwa kuendelea kulinda ustawi wa soko la ndani. 
Baadhi ya Watumishi na wadau wa Sekta ya Anga wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa mamlaka hio pamoja na wadau wa usafiri wa Anga mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa sekta ya Anga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad