HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 26, 2024

VIJIJI 14 VYA SIMANJIRO NA KUNUFAISHWA NA UCRT

 

Na Mwandishi wetu, Simanjiro
VIJIJI 14 vya jamii ya jamii ya wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro na Kiteto Mkoani Manyara, vitanufaika na mradi wa uhifadhi jumuishi wa mazingira na kuboresha maisha ya jamii.

Jamii ya wafugaji wa vijiji hivyo watanufaika na mradi huo wa miaka minne unaoanza mwaka 2024 na kumalizika 2027 utasimamiwa na shirika la Ujamaa Community Resource Team (UCRT).

Mratibu wa UCRT Edward Loure ameyasema hayo mji mdogo wa Orkesumet kwenye uzinduzi wa mradi huo uliofanywa na mkuu wa wilaya hiyo Suleiman Serera.

Loure amesema kwa wilaya ya Simanjiro mradi huo unatarajia kulenga vijiji vya Ruvu Remit, Lerumo, Ngage, Loiborsoit B, Gunge, Lemkuna, Lengasiti, Losoito na Naisinyai.

“Kwa upande wa wilaya ya Kiteto vijiji vitakavyonufaika na mradi huu ni Makame, Ngabolo, Irkiushioibor, Katikati na Ndedo,” amesema Loure.

Amesema lengo kuu la mradi ni ulinzi milki za ardhi za jamii, kujengea uwezo taasisi za vijiji, ili kuweza kusimamia, kutumia na kunufaika na rasilimali maliasili katika msingi endelevu.

“Malengo tarajiwa ya mradi ni ulinzi wa ardhi za vijiji kisheria kupitia vyeti vya ardhi vya vijiji, mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na hati za haki miliki za kimila kwa maeneo ya malisho,” amesema Loure.

Ametaja malengo mengine ya mradi huo ni usimamizi na matumizi endelevu wa rasilimali maliasili katika misingi endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

“Pia jamii kunufaika na rasilimali maliasili zinazowazunguka kupitia miradi iliyorafiki na mazingira, ili kuendeleza jitihada za uhifadhi unaojali mahitaji ya jamii na bioanuai katika ikolojia mbalimbali,” amesema.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Dk Suleiman Serera amesema Loure ni miongoni mwa wakazi wa eneo hilo wanaotumia elimu kwa lengo la kunufaisha jamii hivyo aungwe mkono.

“Loure ni mwana mazingira bora duniani ambaye anawajali wana Simanjiro kwani mara nyingi amekuwa akiandika miradi mbalimbali yenye,” amesema Dk Serera.

Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema Loure kupitia shirika la UCRT amewezesha upimaji na kupatikana kwa hati kwenye vijiji zaidi ya 30 vya Simanjiro.

“Umekuwa ukijulikana wewe binafsi kama taasisi hivyo tutaendelea kukuunga mkono kwani umenufaisha vijiji kupanga matumizi bora ya ardhi,” amesema Ole Sendeka.

Mkazi wa kata ya Ruvu Remit Mokia Mirimba amesema wadau kama Loure wanaendelea kuwaunga mkono kwani wamejitolea kwa hali na mali kusaidia na kunufaisha jamii.

“Mwana mazingira Loure ni mwana maendeleo mzuri kwa hapa kwetu Simanjiro kutokana na mchango wake mkubwa anaoutoa kila mara tunapaswa kumpongeza,” amesema

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad