HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 23, 2024

Tanzania na Kenya zakubaliana kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru

Tanzania na Kenya zimekubaliana kuendelea kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru kwa kuwa na Mpango wa pamoja wa kuwianisha tozo, ada , ushuru, ada na sheria au taratibu zinazoathiri biasharabaina ya pande hizi mbilmasharti mengine yanayoathiri biashara pamoja na kuwezesha ufanyaji biashara mpakani kwa saa 24 ili kukuza biashara baina ya nchi hizo kila siku, kila mwezi na kila mwaka.

Aidha, amebainisha kuwa Nchi hizo zimekubaliana kuhakikisha kuwa .Sheria za Tanzania hazizuii wafanyabiashara wa Kenya kufanya biashara Tanzania na Sheria za Kenya hazizuii wafanyabiashara wa Tanzania kufanya biashara nchini Kenya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akiwa na Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano baada ya kusaini na kukabidhiana Tamko la Pamoja la Makubaliano ( Communique) wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024

Akifafanua zaidi kuhusu makubaliano yaliyotiwa saini , Mhe Byabato amesema Mkutano huo ulitambua kuwa katika siku 30 zilizopita, baadhi ya vikwazo visivyo vya kiushuru vimeondolea ili kukuza biashara na uchumi baina ya nchi hizo kwa kasi na kuimarisha uhusiano na Kenya ambayo ni Mshirika muhimu wa kibiashara wa Tanzania.

Amesema vikwazo hivyo ni pamoja na kuruhusu kuondolewa kwa zuio la kuingiza chai nchini kutoka Kenya, kuondolewa kwa zuio la kuingiza pombe aina ya Konyagi kwenda nchini Kenya, kuondolewa kwa zuio la kusafirisha mbao kwenda Kenya kupitia mpaka wa Horohoro uliokuwa umezuliwa na Shirika la Viwango nchini Kenya

Naye Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano amesema Kenya iko tayari kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru ili kukuza biashara na uchumi pamoja na kuimarisha umoja wa wananchi wa nchi zote mbili

Aidha amebainisha kuwa Nchi hizo mbili zimekubaliana kushughulikia baadhi ya vikwazo kwa njia za kiutendaji na mamlaka mbalimbali kutoka pande zote mbili na kuimatisha utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa makubaliano na kubadilishana taarifa kuhusu maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizo.

Mkutano huo wa nane ni utekelezaji wa Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto yaliyolenga kuondoa vikwazo vyote vinavyoathiri biashara ili kuimarisha uhusiano wa biashara

Aidha, Mkutano huu wa nane ulilenga kushughulikia vkiwazo vilivyobaki katika Mkutano wa Saba wa Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika tarehe 9-12 Machi 2022 huko Zanzibar na unatarajiwa kufanyika Julai 2024 ukilenga kupunguza au kuondoa kabisa vikwazo vilivyobaki ili kukuza biashara na uchumi wa nchi zotw mbili.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akiwa na Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano (waliokaa) wakisaini Hati za Makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru baina ya Kenya na Tanzania wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024.


Wanaoshuhudia wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya Mhe. Peninah Malonza,waliosimama nyuma yao ni Makatibu Wakuu wanaohusika na uwekezaji, viwanda biashara wa nchi zote mbili, Katibu Mkuu wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mabalozi wa Tanzania nchini Kenya.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato na Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya Mhe. Rebbecca Miano (waliokaa) wakikabidhiana Hati za Makubaliano ya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru baina ya Kenya na Tanzania wakati wa Mkutano wa nane (8) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya Tanzania na Kenya ngazi ya Mawaziri uliofanyika Kisumu nchini Kenya tarehe 22/03/2024.


Wanaoshuhudia wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda wa Kenya Mhe. Peninah Malonza,waliosimama nyuma yao ni Makatibu Wakuu wanaohusika na uwekezaji, viwanda biashara wa nchi zote mbili, Katibu Mkuu wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Mabalozi wa Tanzania nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad