HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 11, 2024

Prof. Lipumba ; Lazima Kuwe na Siasa Zenye Hoja na Sera zenye Maendeleo

 

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza wakati wa kufungua kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana. Majadiliano hayo yamefanyika  leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Confucious, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) Bernadetha Kafuko akizungumza wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana. Majadiliano hayo yamefanyika  leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Confucious, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam.
Joseph Selasini akielezea uzoefu wake katika siasa na namna alivyoingia katika siasa  wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana. Majadiliano hayo yamefanyika  leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Confucious, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, John Mnyika akielezea uzoefu wake katika siasa na namna alivyoingia katika siasa  wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana. Majadiliano hayo yamefanyika  leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Confucious, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana, ACT WAZALENDO, Abdul Nondo akiuliza swali katika siasa na namna alivyoingia katika siasa  wakati wa kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana. Majadiliano hayo yamefanyika  leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Confucious, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) Profesa Ibrahim Lipumba amesema lazima kuwe na siasa zenye hoja na Sera kwa sababu watu hawasimamiwi bali utatuzi wa matatizo yanayoikabili nchi, kwa misingi ya kukuza uchumi, kutokomeza umaskini na kujenga misingi imara kwa wananchi wote, tukiwa na msingi bora wa demokrasia.

Ameyasema hayo leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Confucious, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam wakati wa kufungua kongamano la Majadiliano rika baina ya Viongozi wa Vyama vya Siasa na Vijana. Amesema kuwa kutakuwa na amani ya kweli na endelevu kwani mjadala huo utawawezesha kubadilishana mawazo kwa lengo la kujenga na kutazama mustakabali wa nchi kwa kutatua matatizo na kujenga Demokrasi.

"Sisi tuna uzoefu na siku za nyuma na tutazungumza hapa, lakini mazungumzo haya yananipa moyo kwa sababu sote tunashiriki kwa hiyo yanaweza kuleta mawazo ya namna gani katika uhalisia tulionao tunaweza kusukuma mabadiliko ambayo yamepitishwa yakawa mabadiliko chanya mpaka tukaweza kuwa na siasa za kidemokrasia na kwamba wapiga kura wakaenda kushiriki kupiga kura na watakayempigia kura, kura hizo

zikahesabiwa na akaambiwa kwamba umepata kura hizo, suala sio nani ameshinda ila suala ni kwamba zile kura zinapopigwa yale matokeo, yawe matokeo ambayo kila mmoja anayaamini." Amesema Prof. Lipumba

Amesema kuwa ameanza kupata wasiwasi kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa utakuwa kama wa mwaka 2019 au utakuwa tofauti? (Hii ni kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Oktoba mwaka huu 2024.)

Prof. Lipumba amewaasa vijana wa Vyama vya Siasa lazima watazame namna ya kushughulikia maendeleo ya nchi yetu.

"Ushiriki wa vijana unahitaji vijana wawe wengi kwa maana ukichukua watu wenye umri wa chini ya miaka 18 ni zaidi ya asilimia 59 ya wananchi wote wa Tanzania na ukichukua watu chini ya umri wa miaka 35 ni karibu robo tatu ya wananchi wote wa Tanzania kwa hiyo hii ni nchi ya vijana na siasa lazima ziwe siasa za kutatua matatizo yanayowakabili vijana.

Amesema kuwa isivyo bahati Tanzania ina siasa za kuunga mkono watu na kuunga mkono fedha, sasa ni lazima kuwe na siasa za hoja na sera kwa sababu viongozi hawasimamii watu bali twanasimamia utatuzi wa matatizo yanayoikabili nchi.

"Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa mbili, moia ni kuweza kukuza uchumi shirikishi utakaotokomeza umaskini ambao umekithiri katika nchi yetu, lakini pili ni suala zima la kujenga misingi ya demokrasia, ili kupata demokrasia ya kweli ni lazima tuone wananchi wanashiriki, wanachagua watu wao ambao watashughulikia tatizo la kwanza la kuweza kujenga, kukuza uchumi." Amesema Prof. Lipumba

Kwa Upande wa Balozi wa Marekani nchini, Michael Battle amesema kuwa hakuna mwenye haki zaidi kuliko mwingine na chama kimoja hadi kingine.

"Tanzaniani yenu (vijana), iwe ni Tanzania Bara au Visiwani, ni yenu."

Akizungumza wakati wa kutoa Uzoefu wake, wakati akizungumza na Vijana, Mwenyekiti wa Chama Cha UDP Taifa, John Cheyo amesema kuwa kwenye Siasa hakuna pesa wenye pesa ni wezi tu hivyo vijana wawe na wajue kiwa kwenye siasa ni kutatua changamoto za kiuchumi zinazoikabili jamii.

"Siasa iwe Part time tu. Ukiutumia muda huo Full time Maisha ya aweza yasiwe mazuri. Muda mwingi uwe vijana fanyeni kazi za kujipatia kipato halali." Amesema Mzee Cheyo.

Kwa Upande wa Joseph Selasini akitoa uzoefu wake katika siasa amewaasa vija kuwa na wito kweli wa kuongoza na kutatua changamoto.

"Usiingie kwenye siasa kama bendera fuata upepo."

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Doroth Them amewaasa vijana kutokuwa na haraka ya maendeleo na kupata uongozi.

Katibu Mkuu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, John Mnyika amesema kuwa vijana wanatakiwa kuwa wavumilivu kwenye siasa kwa wananchi kwa sasa wanataka viongozi Vijana hivyo wameaswa kuwa na Sera ambazo zitakuwa na msaada kwa jamii husika.

Pia amewaasa vijana ambao wamejaliwa fedha na wasiojaliwa wasiache kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani wataongoza watu na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad