HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 29, 2024

Miaka kumi ya mabadiliko ya kimfumo katika usimamizi na uthibiti wa taka nchini Tanzania

  


Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri Duniani, tunajivunia kuadhimisha miaka 10 ya mabadiliko ya kimfumo katika usimamizi na uthibiti wa taka nchini Tanzania!

Udhibiti wa taka unaonyesha ukosefu wa usawa wa kijamii katika kanda mbalimbali, ambapo jamii nyingi za kipato cha chini hazina huduma za usimamizi wa taka na hupambana na matokeo ya uchafuzi wa mazingira ambayo ina athari kubwa kwa afya na maisha yao. Vikundi vilivyo katika mazingira hatarishi, kama vile wanawake, vijana, wakusanya taka, na wakazi wa kiasili lazima wajumuishwe katika suluhu za usimamizi wa taka na wapate fursa, kupitia jukumu hilo, kurejesha hadhi yao husika ya kijamii.

Udhibiti wa taka ni moja ya masuala muhimu ya mazingira ya Tanzania. Miji inayokua kwa kasi sana ina uwezo duni wa kukusanya na kuthibiti taka. Hili husababisha kiasi kikubwa cha taka ngumu zisizokusanywa kutupwa katika sehemu mbalimbali katika miji yote. Sekta ya taka ndiyo mchangiaji mkuu wa uzalishaji wa gesi ya ukaa nchini Tanzania huku taka za ozo zikiwa mchangiaji mkuu wa uzalishaji wa methane kutokana na utupaji taka katika dampo la wazi. Utafiti wa “Zero Waste to Zero Emissions” uliongazia jiji la Dar es Salaam (uk. 54) unaonyesha kuwa utekelezaji wa mfumo wa Taka Sifuri unaweza kupunguza uzalishaji wa gasi ya methane kwa 65% na idadi hii inaweza kusambazwa nchi nzima.

Leo tumezindua Makala ya mfumo wa Taka Sifuri hapa Kituo cha kupokea na kuchakata taka Bonyokwa. Kupitia maonyesho haya, tunalenga kueneza ujumbe wa mfumo wa Taka Sifuri, kushirikiana na serikali, jamii, na wadau wa mazingira kuangazia hatua muhimu ambazo tumefikia pamoja tangu 2019.

Akifungua maonyesho haya mgeni rasmi, Mh. Saady Khimji ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za jamii jiji la Dar es salaam alisema, “Nimefurahishwa sana na kazi nzuri ushirika wa waokota taka wanayoifanya hapa Bonyokwa. Mazingira ni masafi sijakutana na vifurushi vya taka pembezoni wala kwenye mitaro wala taka zilizozagaa hovyo. Ningeomba Taasisi ya Nipe Fagio tushirikiane kwa pamoja ili kuupeleka mfumo huu katika kata zote za Ilala.”

Wilyhard Shishikaye, Mratibu wa Mradi wa Sifuri wa Taka Tanzania kutoka taasisi ya Nipe Fagio alisema "Katika miaka mitano (5) ya utekelezaji wa Taka Sifuri, Nipe Fagio imeweza kutekeleza mifumo ya Taka Sifuri mikoa mitatu (3) ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha na Zanzibar."

Aliongeza, “Tumesajili chama cha ushirika cha kwanza kuwahi kutokea nchini cha Wakusanya Taka Bonyokwa kilichopo Bonyokwa Dar Es Salaam chenye wanachama zaidi ya 26, hivyo kutengeneza historia kwa vyama rasmi vya wakusanya taka na kuwa daraja kati ya kutambulika rasmi na kazi zao.”

Kuanzia mitaa yenye shughuli nyingi za Dar es Salaam hadi mandhari tulivu ya Arusha na mwambao mahiri wa Zanzibar, Mfumo wa Taka Sifuri umekuwa ukichochea mabadiliko ya mfumo katika usimamizi wa taka. Kupitia mfumo huu tumefikia kiwango cha 95% cha utenganishaji wa taka katika maeneo ya Dar es Salaam na Arusha. Hii ina maana kwamba 95% ya watu wanaoishi katika jamii za kipato cha chini wamekubali kutenganisha taka zao katika makundi yaliyoamuliwa awali kuwezesha viwango vya juu vya kurejesha taka.

John Yusuph Nsyenge, Mwenyekiti wa Wakusanya Taka Bonyokwa alisema, “Tumeweza kurejesha 75-85% ya taka zote zinazozalishwa katika ngazi ya kaya kupitia mboji, uzalishaji wa chakula cha mifugo na urejelezaji. Tumeweza kuthibiti wastani wa tani 39 za taka kwa mwezi katika kila Mtaa tunachohudumia, ambapo tani 30 ni taka ozo.”

Ajira: Ajira zaidi ya 33 katika sekta ya taka kwa jiji la Dar es Salaam ziliongozeka.

Ubunifu: Tumetengeneza “application” ya ukusanyaji wa ada za taka ambayo hutuma kieletroniki uthibitisho wa malipo kwa kaya kupitia ujumbe mfupi (SMS), kuongeza uwazi wa mfumo na kupunguza ulaghai. Tulitoa huduma za udhibiti wa taka kwa jamii ambazo hazikuwa na ufikiaji wa huduma za usimamizi wa taka kwa kutumia chini ya 15% ya makadirio ya bajeti ya usimamizi wa taka kwa manispaa.

Ushirikiano: Kuendeleza ushirikiano, tumeweza kuwaleta pamoja watoa huduma, wakandarasi, warejelezaji na wakusanyaji taka za kibiashara kwa kuunganisha na muundo wa kukusanya taka ambao unaendana na mfumo wa taka sifuri na kuongeza ufanisi wa mfumo.

Ushawishi wa Serikali: Tulipokea ahadi kutoka kwa serikali ya Zanzibar ya kuondoa ushuru na ada za ukusanyaji taka kutoka kwa vyama vya ushirika vya ukusanyaji taka.

Nje ya Mipaka: Kutokana na matokeo chanya ya mfumo wa Taka Sifuri hapa Tanzania, nchi ya jirani Kenya wameweza kuiga Mfano huu kwa kuanza kutekeleza mfumo huu huko Kisumu.

Mtandao wa Taka Sifuri: Tumezindua mafunzo rasmi ya kwanza ya Taka Sifuri yaliyohususha watekelezaji wa mfumo huu kutoka bara la Afrika, tuliopata waombaji zaidi ya 150 kutoka nchi 25 tofauti ulimwenguni.

Mfumo wa Taka Sifuri unaotekelezwa nchini Tanzania ni jitihada za wazi la jinsi mifumo ya kijamii inavyoweza kuigwa kwa mafanikio na kuingizwa katika mazungumzo ya kitaifa, kukuza haki ya kijamii, na kuleta mabadiliko katika utekelezaji katika miji na nchi nyingi za Afrika. Mfumo huu ni kielelezo kamili, chenye manufaa katika uzalishaji wa ajira, kukabiliana na hali ya hewa, kuongeza ufahamu na haki ya kijamii.

Ana Rocha, Mkurugenzi Mtendaji alihitimisha, "Watu wanapopewa uchaguzi mzuri, wanauchukua. Taka Sifuri sio suluhisho tu; ni dhamira ya mustakabali shirikishi kwa Tanzania, jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko.”

Aliongeza, "Mfumo wa Taka Sifuri unapendekeza mifumo itakayotatua matatizo ya kimazingira kama Uchafuzi wa hali ya hewa, kuruhusu jamii kuelewa mienendo yake na kuchukua hatua stahiki katika kushughulikia matatizo yao. Mfumo huu unaotekelezwa nchini Tanzania ni jitihada za wazi unaoshirikisha jamii wenye mafanikio unavyoweza kuigwa kwa mafanikio na kuingizwa katika mazungumzo ya kitaifa, kukuza haki ya kijamii, na kuleta mabadiliko katika utekelezaji wa usimamizi wa taka katika miji na nchi nyingi za Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad