HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 7, 2024

Hospitali ya Kitonka Yamshinda Mgonjwa Wake Mahakamani

 Na Mwandishi Wetu
HOSPTALI ya Kitonka ya Gongolamboto jijjnj Dar es Salaam imeshinda kesi ya uzembe iliyofunguliwa na mgonjwa wake, Mwalu Dege akiidai fidia ya Sh. Milioni 700 kutokana na kile alichodai uzembe uliofanywa katika matibabu yake.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Salma Maghimbi akisema kuwa mdai huyo ameshindwa kuithibitishia mahakama ni uzembe gani kitaaluma uliofanywa na Hospitali hiyo (mdaiwa) na kumsababishia madhara kama alivyodai.

Jaji Maghimbi amesema kwamba kulingana na matatizo aliyokuwa nayo mdai na matokeo ya uchunguzi wa awali hatua zilizochukuliwa na hospitali hiyo yaani matibabu kwa njia ya upasuaji zilikuwa ni muhimu Kwa ajili ya kuokoa uhai wake.

Amesema kuwa shahidi wa pili upande wa madai (mgonjwa) dakatri wa Muhimbili wakati alipohojiwa na Wakili wa mdaiwa (Hospitali ya Kitonka) alieleza kuwa baada ya uchunguzi kwa kutumia MRI walibaini kuwa hapakuwa na uharibifu kwenye mfuko wa uzazi wa mdai.

Jaji Maghimbi amesema kuwa ushahidi huo unakinzana na madai ya mdai na kwamba huo unatosha kumsafisha mdaiwa katika madai ya uzembe.

"Hapakuwa na uzembe wa kitaaluma kwa upande wa mdaiwa uliyosababisha mdai kufanyiwa taratibu za matibabu zisizo za umuhimu. Mdai hastahili kulipwa fidia, hivyo kesi hiyo imefutiliwa mbali."amesema Jaji Maghimbi baada ya kujadili ushahidi wa pande zote.

Katika kesi hiyo namba 134 ya 2022 Mwalu aliwakilishwa na wakili wa kujitegemea, Gadi Silas huku mdaiwa (Hospitali ya Kintoka) ikiwakilishwa wakili Cheba Kameya kutoka kampuni ya Acero Legal Consultancy.

Katika madai yame Mwalu aliiomba Mahakama hiyo iiamuru Hospitali ya Kitonka imlipe fidia ya Sh. Milioni 700 akidai kuwa kuna uzembe uliofanywa katika matibabu na kumsababishia kufanyiwa upasuaji usio sahihi kutoa ujauzito wake na kumsababishia ulemavu wa kudumu, kutokana na madhara waliyomsababishia katika mfuko wa uzazi.

Kwa mujibu wa hati ya madai yake Mwalu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la maumivu ya tumbo huku akotokwa na damu nyingi, wakati akiwa na ujauzito na Februari 26,2022 alikwenda katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.

Hospitalini hapo alifanyiwa vipimo na majibu yalipotoka aliambiwa mimba imetungwa nje ya mfuko na kwamba ana uvimbe kwenye tumbo lake hivyo anatakiwa afanyiwe upasuaji.

Yeye na mumewe waliomba wakafanye vipimo vingine zaidi sehemu nyingine Ili kujiridhisha na majibi hayo lakini daktari hiyo alimsisitiza kuwa ilikuwa ni muhimu afanyiwe upasuaji huo ili kuokoa uhai wake, nao wakakubali.

Baada ya kufayiwa upasuaji huo alilazwa siku tano kwa ajili ya uangalizi lakini aliendelea kupata maumivu makali ya tumbo huku akitokwa na damu nyingi.

Hivyo alimtafuta daktari aliyemfanyia matibabu hayo ambaye alimweleza kuwa wakati anamfanyia hakuona kitu chochote kama ilivyodaiwa.

Baada ya hali kuzidi kuwa mbaya waliomba rufaa akapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (NMH), ambako daktari aliyemhudumia alimweleza kuwa ingawa kweli alikuwa na tatizo lakini hakupaswa kufanyiwa huduma ya upasuaji haraka

Kwa mujibu wa daktari wa aliyemhudia Muhimbili, ilibainika kuwa wakati alipofanyiwa upasuaji alikuwa na tatizo katika mfuko wa uzazi, hata hivyo waliurekebisha na kurudisha katika hali yake ya kawaida.

Daktari huyo aliieleza Mahakama kuwa kwa maoni yake aliona kama tatizo lililokuwepo lilitokana mimba iliyoshindikana kutoka na kwamba tiba yake ilikuwa ni kuiondoa na kwamba katika hali hiyo yeye asingetumia njia ya upasuaji.

Hata hivyo hospitali hiyo ilipinga madai hayo ikidai kuwa yote yaliyofanyika yalikuwa ni kuhakikisha kuwa inaokoa uhai wake, Mwalu na kwamba hapakuwa na uzembe wowote.

Ilidai kuwa hakulazimishwa bali alishauriwa kuwa hiyo ndio ilikuwa namna bora ya kuondoa tatizo lake na aliridhia akasaini na kwamba taratibu zote za kitabibu zilizingatiwa kwa kiwango cha hali ya juu kiasi kwamba hakuna madhara makubwa au ulemavu wa kudumu uliojitokeza.

Katika hukumu hiyo Jaji Maghimbi amesema kuwa baada ya kusikikiza ushahidi wa pande zote, ni dhahiri Mwalu aliridhia taratibu hizo za matibabu.

Amesema kuwa kwa mujibu wa ushahidi wa pande zote Mwalu alikuwa na tatizo ambalo hatima yake ilikuwa ni kuondoa ujauzito aliokuwa nao na kwamba kwa mujibu ushahidi huo tofauti ilikuwa ni njia gani itumike kuuondoa.

Hivyo amesema kuwa ameridhika kuwa kulingana na hali aliyokuwa nayo na tatizo lililoonekana awali njia ya upasuaji iliyopendekezwa na kuchukuliwa na daktari wa hospitali hiyo ilikuwa ni muhimu kuokoa uhai wake na hakuna sababu ya kumlaumu daktari huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad