HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 7, 2024

HALOTEL TANZANIA KUSHEHEREKEA SIKUUKUU YA WANAWAKE KWA KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA MALAIKA.

 Halotel kuonesha dhamira yao katika kujali jamii iliweza kutembelea kituo cha watoto yatima cha Malaika kilichopo Mwananyama - Mango Garden katika kukaribisha sherehe za sikuukuu ya Wanawake mwaka 2024.

Halotel Tanzania ilikusanyika katika kituo cha watoto Yatima Malaika kilichopo Mwananyamala – mango Garden ili kuweza kuwatembelea watoto ambao wapo kwenye hiko kituo. Katika kuheshimu na kukaribisha sikuukuu ya wanawake na kutambua umuhimu wa mwanamke katika jamii yetu Halotel imeamua kuwashika mkono wanawake ambao wameazisha kituo hiki cha watoto Yatima Malaika.

Katika ujio wao, Halotel Tanzania iliweza kujumuika na watoto hawa katika michezo mbalimbali ya kujifunza. ‘Tunaamini katika nguvu ya kujali na kurudisha katika jamii hususani kwenye siku kubwa kabisa ya sikuukuu za wanawake’ alisema Madam Sharon Kessy Afisa kutoka kitengo cha Huduma kwa wateja. ‘Kwa kuwatembelea watoto hawa tunatambua umuhimu wa kuwaelimisha na kuwatia moyo kujikita katika elimu ili kuweza kujikwamua katika maisha.’ Aliendelea Madam Sharon.

Halotel Tanzania kwa kutembelea Kituo hiki inaendelea kuonesha dhamira yao katika kujali jamii. Halotel Tanzania iligawa Zaidi ya mifuko 600 ya Mchele, vifaa vya usafi, Taulo za kike vikiwemo ni vitu vichache kati ya vingi walivovitoa. Vitu hivi vilikabidhiwa kwa wanawake wanaosimamia kituo hiki cha watoto yatima cha Malaika.

Halotel Tanzania inapenda kuwashukuru na kuwatia moyo wanawake wanaosaidia watoto hawa katika hiki kituo cha watoto Yatima cha Malaika, lakini pia kuwatia moyo wanawake wote wanaojitahidi kujishughulisha kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali katika jamii Yetu.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad