HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 24, 2024

DKT. TULIA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 148 WA IPU GENEVA

 

RAIS wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha CICG, Geneva nchini Uswisi leo tarehe 24 Machi, 2024.



Mkutano huo unatarajiwa kujadili Dhima Kuu ambayo ni “Matumizi ya Diplomasia ya Kibunge katika kuleta Amani na Maelewano Duniani”. Mkutano huo umehudhuriwa na Maspika wa Mabunge 48 na washiriki zaidi ya 1,500. Mkutano huo unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27 Machi, 2024.
PICHA NA OFISI YA BUNGE

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad