HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 27, 2024

BFT LATANGAZA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA ITAKAYOWAKILISHA TAIFA KWA MICHEZO YA AFRIKA ACCRA GHANA

 

SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA (BFT) LATANGAZA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA ITAKAYOWAKILISHA TAIFA KWA MICHEZO YA AFRIKA TAREHE 15.03.2024 ACCRA GHANA.
Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) leo limetangaza kikosi cha timu ya taifa ya ngumi, yenye jumla ya mabondia 8 na walimu 2. Kati ya hao mabondia wanaume ni 6 na wanawake 2. Kikosi hicho kitawakilisha taifa katika mashindano ya ngumi ya Afrika yatakayofanyika kuanzia tarehe 15-23/03/2024,Accra Ghana.

Timu hiyo inatarajia kuondoka hapa nchini tarehe 09/03/2024 kuelekea Ghana. Mabondia waliochaguliwa ni kama ifuatavyo:-
Wanaume

1. Yusuf Changalawe 81Kg.
2. Abdallah Mohamed 51 Kg.
3. Adallah Mfaume 67Kg.
4. Ezra Paul 60Kg.
5. Mussa Maregesi 86Kg.
6. Mhina Magogo 92Kg.

Wanawake.
1. Zulfa Macho 52Kg.
2. Miriam Maligisa 48Kg.

Makocha
1. Samweli Kapungu
2. Muhisin Mohamed.

Aidha bondia Lucas Changalawe aliondoka jana kuelekea Italy kushiriki katika mashindano ya kufuzu kushiriki Olimpiki yatakayofanyika kuanzia tarehe 01-11 Mar 2024.

Baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ya Italy bondia Lucas Changalawe atalazima kusafiri kuelekea Ghana kushiriki pia michezo ya Afrika.

Tunaitakia kheri timu yetu ya taifa ya ngumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad