HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 17, 2024

Benki ya Absa yaendelea kuwawezesha wanawake kiuchumi.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum (kulia), akikabidhi tuzo ya shukrani kwa Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Mwilongo Irene Msungu ( katikati ) kwa kutambua mchango wa benki hiyo kama  mdhamini Mkuu katika uzinduzi wa Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha Tanzania (TAWiFA), wakati wa hafla iliyofanyika, Kizimkazi, Zanzibar jana. Kushoto ni Meneja wa Absa Tawi la Zanzibar, Bi. Rabia Aboud.Hii ni moja ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwezesha wanawake kiuchumi  sambamba na akaunti maalumu Ya wanawake ya  Absa She account, iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo haina ada za mwezi wala makato ya miamala.

Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Mwilongo Irene Msungu (kushoto), akipokea tuzo ya shukurani kutoka Kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dk. Saada Mkuya Salum, Kwa kutambua mchango wa Absa kama mdhamini mkuu katika uzinduzi wa Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha Tanzania (TAWiFA), wakati wa hafla iliyofanyika Kizimkazi, Zanzibar jana. Mbele kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi. Hii ni moja ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwezesha wanawake kiuchumi  sambamba na akaunti maalumu Ya wanawake ya  Absa She account, iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo haina ada ya mwezi wala makato ya miamala.

Mjane wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Bi. Fatma Karume ( kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. mwilongo Irene Msungu ( kulia ) na Meneja wa Absa Tawi la Zanzibar, Bi. Rabia Aboud,  wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha Tanzania (TAWiFA), uliodhaminiwa na Benki ya Absa na kufanyika mjini Kizimkazi, Zanzibar jana. Hii ni moja ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwezesha wanawake kiuchumi  sambamba na akaunti maalumu Ya wanawake ya  Absa She account, iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo haina ada ya mwezi wa makato ya miamala.

Baadhi ya washiriki  wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha Tanzania (TAWiFA) uliofanyika, Kizimkazi, Zanzibar jana. Benki ya Absa ilikuwa mdhamini mkuu wa uzinduzi huo.Hii ni moja ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwezesha wanawake kiuchumi  sambamba na akaunti maalumu ya wanawake ya  Absa She account, iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo haina ada ya mwezi wala makato ya miamala.

Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Mwilongo Irene Msungu (wa tatu kushoto) na Meneja wa Absa Tawi la Zanzibar, Bi. Rabia Aboud ( wa tatu kulia ) wakionyesha tuzo iliyopewa benki hiyo, kama mdhamini mkuu katika hafla ya  uzinduzi wa Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha Tanzania (TAWiFA), uliofanyika, Kizimkazi, Zanzibar jana.Hii ni moja ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwezesha wanawake kiuchumi  sambamba na akaunti maalumu Ya wanawake ya  Absa She account, iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo haina ada ya mwezi wala makato ya kufanya miamala.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad