HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 6, 2024

ATE YAHITIMISHA MAFUNZO YA MWANAMKE KIONGOZI AWAMU YA TISA

 


Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Dk Dorothy Gwajima ametoa wito kwa kwa jamii kuendelea kutumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili wa jinsia sambamba na kuwalinda wanawake na watoto.

Amesema ni muhimu kuwekeza kwa wanawake, kwani kwa kufanya hivyo, ni kuongeza kasi ya maendeleo, kukuza ustawi wa jamii, na kujenga familia bora kwa maslahi ya taifa .

Dk Gwajima ameyasema hayo leo Machi 6,2024 kwenye hafla ya kuhitimisha mafunzo ya mwanamke kiongozi awamu ya tisa yaliyoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).

Mafunzo hayo yamehusisha wahitimu 497 yaliyolenga kuwajengea uwezo wanawake kumudu nafasi za juu za uongozi.

Amesema Shirika la Umoja wa Mataifa linashoghulikia masuala ya Wanawake (UN Women), limeeleza vitendo vya ukatili wa dhidi ya wanawake hugharimu asilimia mbili ya uchumi wa dunia na Ripoti ya Benki ya Dunia ikionyesha baadhi ya nchi hutumia hadi asilimia 3.5 ya pato ghafi la ndani kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia.

“Kwa takwimu hizi ni dhahiri kwamba, hatutaweza kusonga mbele ikiwa tutaendelea kufumbia macho masuala haya,”amesema.

Pia ameeleza kuwa “Wanawake tushiakamane kwamba, ninyi mliopo maeneo ya kazi, muwanyanyue na wengine, muwasaidie, msiwe visababishi vya misongo ya mawazo kwa wengine."

Ameeleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na ATE kuhakikisha kunakuwa na rafiki ya ushiriki wa wanawake katika nyanja mbali mbali za kiuchumi, ili kukuza uchumi wa nchi na wananchi wote.

Kwa upande wake, Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Patrobas Katambi amesema shida kubwa ya maadili ipo kwa watoto wa viongozi ambao hata nafasi za ajira zinapotoka hawataki kushindana wengine wanaziomba nafasi hizo kwa barua ya maelekezo ‘memo’

Katambi amesema taifa linakosa viongozi kutokana na mmomonyoko wa maadili akidokeza wazazi kuwa bize na mambo yao badala ya kujali makuzi na malezi ya familia.

“Usiwaachie wasaidizi wa ndani kuwa wazazi,wanawake mliopo hapa ujuzi na maarifa mliopewa, fedha tunazotafuta nyumba na magari hazina maana, takwimu nilizonazo watoto wengi wa viongozi wanaharibikiwa sana hata nafasi za ajira zikitoka hawataki kujituma wanakwenda kusema baba amenituma,”amesema.

Ameongeza kuwa watoto wamekuwa wakilawitiwa kutokana na ubize wa wazazi kutokana na kuwaachia wasaidizi wa ndani kila kitu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk Suzan Ndomba amewataka wanawake waliopewa mafunzo ya uongozi kutumia maarifa waliyopewa kuleta mabadiliko na kuwabadilisha wengine.

Akidokeza suala la usawa kijinsia alisema kampuni zote zilisosimamia usawa wa kijinsia zimepata faida.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Doroth Gwajima leo Machi 06, 2024 akifurahia baada ya kumgawia cheti ya kuhitimu mafunzo ya mwanamke kiongozi mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo wakati kuhitimisha mafunzo ya Mwanamke kiongozi awamu ya tisa yaliyoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) yaliyohusisha wahitimu 497. Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wanawake kumudu nafasi za juu za uongozi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Doroth Gwajima akizungumza leo Machi 06, 2024 wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya Mwanamke kiongozi awamu ya tisa yaliyoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) yaliyohusisha wahitimu 497. Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wanawake kumudu nafasi za juu za uongozi.
Naibu Waziri, ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu) Patrobas Katambi akizungumza leo Machi 06, 2024 wakati wa hafla ya ya kuhitimisha mafunzo ya Mwanamke kiongozi awamu ya tisa yaliyoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) yaliyohusisha wahitimu 497. Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wanawake kumudu nafasi za juu za uongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Suzan Ndomba akizungumza leo Machi 06, 2024 wakati wa hafla hiyo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Mwanamke kiongozi awamu ya tisa yaliyoratibiwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) yaliyohusisha wahitimu 497.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad