Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC) kinaendesha kozi ya kuwajengea Uwezo wa Kiukaguzi ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 12 kutoka nchini Tanzania na Somalia ya yenye lengo la kuziwezesha nchi za Afrika katika masuala ya Usalama wa Usafiri wa Anga.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga (DSR) Mgeni rasmi Kaimu DSR Furaha Sanga amewataka washiriki wa kozi hiyo kwenda na kufundisha wengine walichojifunza kwa manufaa ya jumuiya nzima ya usafiri wa anga.
Sanga amewashukuru washiriki hao wa kozi hiyo kwa kuichagua CATC ambayo pia ni moja katika vyuo vya mafunzo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga(ASTC) kuwa sehemu ya kufanyia mafunzo yao hayo.
Ufunguzi huo pia ulihudhuriwa na mwakilishi wa Ubalozi wa Somalia nchini Bw.Yassin Arale na Didacus Mweya Mkuu wa mafunzo CATC.
CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Furaha Sanga akizungumza wakati wa kufungua kozi hiyo kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 12 kutoka nchini Tanzania na Somalia iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Mweya Didacus akizungumza kuhusu kazi zinazofanywa na chuo hicho wakati wa kufunga kozi hiyo ya siku tano kwa wakaguzi wa Usafiri wa Anga 12 kutoka nchini Tanzania na Somalia iliyofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya(ECAC).
Baadhi ya wakaguzi wa Usafiri wa Anga 12 kutoka nchini Tanzania na Somalia wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Furaha Sanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari.
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usalama wa Usafiri wa Anga Furaha Sanga akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), wakufunzi kutoka Tume ya Usafiri wa Anga ya Ulaya (ECAC) na wakaguzi wa Usafiri wa Anga 12 kutoka nchini Tanzania na Somalia mara baada ya kufungua iliyofanyika kwa siku tano yenye lengo la kuziwezesha nchi za Afrika katika masuala ya Usalama wa Usafiri wa Anga.
No comments:
Post a Comment