HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 9, 2024

WAKUFUNZI WA VITUO VYA KUFUNDISHIA MITIHANI YA BODI WAPIGWA MSASA


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA) imeendesha warsha kwa njia ya mtandao kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ili kuwaongezea ujuzi.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema lengo la warsha hiyo ni kuwakumbusha majukumu yao ili kuendana na mitaala wa Bodi.

Maneno amesema mafunzo ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia mwaka huu yamekuja na mabadiliko ya mitaala ya masomo ya Bodi hivyo amewataka kujadili vyema ili wanapokwenda kutoa elimu wawe na uelewa mzuri.

Pia amesema lengo kubwa la NBAA ni kuona wanapandisha kiwango cha ufaulu kwa mitihani mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya Uhasibu na Ukaguzi.

Amewaasa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia masomo ya Bodi kuendesha masomo kwa njia ya mtandao ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji, kuwafikia wanafunzi wengi na kuendana na teknolojia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza wakati wa kufungua warsha ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi iliyofanyika katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo (kulia) akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa warsa hiyo pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno kwa ajili ya kufungua warsha hiyo kwa njia ya mtandao.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria NBAA, Agnes Kessy akitoa mada kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi  kuhusu sheria mbalimbali za Bodi kwa wanafunzi wanaobidi kufanya Mitihani  katika warsha iliyofanyika  katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa maelezo na muongozo wa warsha ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi iliyofanyika katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mthibiti Ubora Mwandamizi kutoka NACTVET Bonaventure Ackles akitoa mada kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi  kuhusu namna nzuri ya kufundishia  wanafunzi kwenye masomo mbalimbali ya Mitihani ya Bodi katika warsha iliyofanyika  katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi CPA Rashid Mganwa akitoa maelezo kuhusu mabadiliko ya masomo ya B2,B3, B4, C3 na C4 nk. kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao.
Afisa Mthibiti Ubora Mkuu - Mitaala kutoka NACTVET Dkt. Edward J. Mneda akizungumza namna ya kutunga Mitihani pamoja na usahihishaji wa Mitihani ya Wanafunzi wa Bodi kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao.
Baadhi ya Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi  wakichangia mada kwenye Warsha ya kuwajengea uwezo wakufunzi hao  katika warsha iliyofanyika  katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mitihani na Usajili kutoka NBAA Heri S. Mnzava akizungumza jambo kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi  wakichangia mada kwenye Warsha ya kuwajengea uwezo wakufunzi hao  katika warsha iliyofanyika  katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa NBAA na Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia Wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi  wakifuatilia mada pamoja na wale wanaofuatilia kwa njia ya mtandao katika warsha hiyo iliyofanyika katika ofisi za  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad