HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 26, 2024

Wadau katika Kili Marathon 2024

Timu ya Uhusiano kwa umma kutoka Kampuni ya Blanq Marketing and Communication Agency ikiongonzwa na Mkurugenzi wake, Asinati Eliafie (kushoto) wamekuwa ni miongoni mwa maelfu ya wakimbiaji walioshiriki mbio za Kili Marathon mkoani Kilimanjaro hapo Jana.

Akizungumza baada ya kutimua mbio hizo za nyika, Asinati Eliafie  amesema wamefanya hivyo ili kuwaunga mkono wateja wao ambao pia wamedhamini mbio hizo na wengine wakiwa tu washiriki wa kawaida.

Anaongeza kuwa anafurahi kuona kazi za wateja wao ambazo zinafanywa na Kampuni yao ya Blanq Marketing and Communication zinawafikia maelfu ya Watanzania.

Mbio hizo zenye hadhi ya kimataifa, zimefanyika Jana kwa kuanza na kumalizika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Moshi mkoni Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad