HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 19, 2024

NIMR Kufanya Utafiti wa Magonjwa Yasiyoambukiza Kwanjia ya Simu

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
TAASISI ya Taifa ya Tafiti za Magonjwa ya Binadamu NIMR kwa kushirikiana na Wizara ya Afya hivi karibuni inatatarajia kuanza kufanya utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza kwa njia ya simu ili kiweza kuwafikia wananchi wengi.

Njia hiyo itasaidia kuwafikia Watanzania wengi kwa muda mfupi na kusaidia kuokoa gharama ambazo zimekuwa zikitumika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 19, 2024 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Prof.Said Aboud amesema NIMR imechagua njia hiyo ili kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi na kwamba suala hilo linawezekana kutokana matumizi ya simu kuwa makubwa nchini.

"Kutokana na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za mkononi, NIMR tumeona ni wakati muafaka kutumia simu za mkononi katika ukusanyaji na uchakataji wa takwimu, kwani itakuwa njia rahisi sana na itaweza kukabiliana na vizuizi vya muda mrefu katika ukusanyaji wa takwimu na ufuatiliaji, hii itasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wakati."

Utafiti huu utatusaidia kufanya tafiti kwa ufanisi wa matumizi ya simu za mkononi kwenye kukusanya taarifa za tafiti nchi nzima na kutuwezesha kuishauri serikali kama matumizi ya tecknolojia yanawezesha upatikanaji wa taarifa sahihi.

Amesema kuwa lengo la kuzungumza na wanahabari ni kuufahamisha umma juu ya kuwepo kwa utafiti huo utakaowashirikisha wanachi moja kwa moja.

"Dhumuni kubwa la kuwaita hapa ni kutusaidia kuwajulisha umma kuhusu utafiti huu utakao anza punde. Wananchi wasisite kushiriki pale watakapokua wamepigiwa simu kushiriki kwenye utafiti huu muhimu. Amesema, utafiti huo utajumuisha sampuli ya wananchi wenye umri kati ya miaka 18 na kuendelea na utafanyika Tanzania Bara pamoja na Zanzibar na unategemea kuchukua wiki 4 mpaka 6.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taarifa na Udhibiti wa Tafiti za Afya, Dkt. Mary Maige pia Mtafiti Mkuu Mwandamizi na Mkurugenzi wa Taarifa za Utafiti Taasis ya Utafiti ya Magonjwa ya Binaadamu NIMR amesema kuwa lengo la utafiti huo ni kuangalia hali ya Magonjwa yasiyoambukiza na viashiria vyake kwa njia ya simu .

"Kawaida tulikuwa tunakwenda nyumba kwa nyumba lakini kwa taifiti za kitaifa tunaona kwamba ile namba ya wananchi tunayokwenda kuifikia ni kubwa na tafiti hizi huwa na gharama"

Amesema kuwa utafiti huo utakaokuwa unaangalia viashiria vya magonjwa unatakiwa kufanywa mara kwa mara ili kubaini na mabadiliko ya mwenendo wa maisha unavyoathiri afya za watu.

"Kwa kuangalia hilo tumeona kuwa hatuwezi kufanya tafiti za nyumba kwa nyumba kwa sababu ya gharama na muda na changamoto ya kuwafikia wananchi wengi hivyo kutumia njia ya simu ni nyenzo muhimu ya kufanya utafiti mara kwa kwa mara" amesema Dkt Maige.

Amesema kuwa ili kudhibiti wahalifu wa mtandaoni watu wataofanyiwa utafiti watatumiwa meseji maalum itakayowafahamisha juu ya kufanyiwa utafiti ili kuepushwa kupigiwa na matapeli.

"hata hivyo kwenye utafiti huo hapatakuwa na gharama zozote zitakowalazimu wananchi kulipa hivyo wakiombwa hela basi wajue hao ni matapeli" amesema Dkt. Maige.

Takwimu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yaliongezeka mara mbili kutoka asilimia 19 mwaka 1990 hadi asilimia 34 mwaka 2015 na yanakadiriwa kuchangia asilimia 33 ya vifo vyote.

Hapa nchini kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023, magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamesababisha wagonjwa wengi kuhudhuria vituo vya huduma za Afya ni pamoja na shinikizo la juu la damu wagonjwa 1,456,881 sawa na asilimia 49 ikilinganishwa na asilimia 34 kipindi kama hicho mwaka 2021/22, kisukari wagonjwa 713,057 sawa na asilimia 24 na magonjwa ya mfumo wa hewa 386,018 sawa na asilimia 13 ikilinganishwa na asilimia 10 kwa kipindi kama hicho mwaka 2021/22.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said S. Aboud  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 202,  juu ya Kuanza Utafiti wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa njia ya simu.
Mkurugenzi wa Taarifa na Udhibiti wa Tafiti za Afya- NIMR, Dkt. Mary Maige  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 19, 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad