HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 8, 2024

Kampuni ya GF Automobile yakabidhi Gari Wizara ya Kilimo kuunga Mkono agenda ya BBT

 

 Kampuni ya GF Automobile wamekabidhi Gari Wizara ya Kilimo ikiwa ni sehemu CSR katika kuunga Mkono agenda ya BBT (Building a Better Tomorrow). 

 
Waziri wa Kilimo , Hussein Bashe amepokea msaada huo wa Gari kutoka kwa GF Automobile LTD Dodoma ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan.

Pia GF Automobile LTD wameamua kutoa msaada ya Gari kwa lengo kuupa Nguvu mradi wa BBT ambao moja kwa moja inafikia Vijana wa Kitanzania na kukuza ajira kupitia Kilimo.

Hayo yameelezwa leo Februari 08,2023 na Mkurugenzi wa Biashara na Masoko GF Group, Bwana Salman Karmali jijini Dodoma

Amesema kampuni ya GF Automobile imeahidi makubwa katika sekta ya Kilimo, kwa kuwa Magari yatakuwa yanaunganishwa hapa Tanzania na yatapatikana kwa Gharama nafuu kwa Tanzania na kuinua Sekta ya Kilimo na kuunga mkono 'Local content'.


"Kampuni ya GF Automobile kwakweli inajipanga kuja na Mapinduzi makubwa katika kuunga mkono sekta ya Kilimo hapa nchini",amesema Bwana Salman KarmaliWaziri wa Kilimo, Husssen Bashe na Mkurugenzi wa Mawasiliano na masoko wa kampuni ya GF Automobile, Salman Karmali (wa pili kulia) wakikata utepe wakati wa  hafla ya  kukabidhi gari iliyotolewa na kampuni ya GF  Automobile  kwa ajili ya mradi wa kilimo BBT wakiwa na lengo ya kuunga mkono seriklia katika sekta ya kilimo wakati wa hafla iliyofanyika  Dodoma. Na mpiga picha maalumuNo comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad