HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 5, 2024

CCM MBEYA YAMALIZA MGOGORO WA SOKO KYELA, WAFANYABIASHARA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO

 

Na. Mwandishi Wetu.

Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa Mbeya Mbeya kikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Patrick Mwalunenge, kimeamua kuingilia kati mgogoro wa muda mrefu wa wafanyabiashara na wamiliki wa soko kuu la Kyela.

Wakizungumza katika Mkutano Maalum wa kutatua Mgogoro huo ambao uliitwishwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya, Ndg.Patrick Mwalunenge, baadhi ya wafanyabiashara wamesema wamiliki wa soko hilo, ambao ni CCM wilaya ya Kyela wamewaondoa ndani ya soko hilo kwa madai ya kupisha ujenzi mpya.

Baada ya mnyukano wa muda mrefu wa kutafuta shuluhu, chama hicho kimekuja maadhimio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu wafanyabiashara ambao waliondolewa walejee sehemu zao za kufanyia bishara kwa kipindi miezi miwili wakati mchakato wa kupata ufumbuzi wa kudumu ukiendelea.

Pia CCM mkoa Mbeya imeshauri kuundwa kwa kamati maalumu ambayo itashirikisha pande zote, yaani wafanyabiashara, wamiliki, wapangaji na mkandarasi alipewa kazi ya ujenzi wa soko hilo ili kuja na majibu namna gani ujenzi mpya wa soko hilo utakuwa shirikiahi kwa pande zote.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ndugu Mwalunenge amesema chama hicho pia kitahakikisha kinafanya ukarabati wa vibanda ambavyo vilibomolewa kwa ajili ya kuanza ujenzi, huku akiahidi kutoa shilingi laki nane Tsh.800,000/= kwaajili ya kuwashika mkono mamantilie wa soko hilo.



 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad