HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 15, 2024

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA ZAWADI KWA GOLIKIPA BORA WA MASHINDANO YA LIGI YA MAPINDUZI CUP VISIWANI ZANZIBAR

 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi cheti maalum kwa Mkurugenzi Mtendajiwa Tanzania Commercial Bank TCB Adam Mihayo mmoja ya wadhamini wa mashindano ya ligi ya Mapinduzi Cup Kwa ikiwa nikutabua na kuthamini uwepo wa wadhamini mbalimbali na wadau wa michezo.
Mkurugenzi Mtendaji waTanzania Commercial Bank PLC(TCB), Adam Mihayo (kushoto), akimkabidhi zawadi ya shilingi 1,000,000/- kwa Mlinda Mlango bora wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023/2024, kutoka Timu ya Mlandege Athuman Hassan, mara baada ya Timu hiyo kuibuka kidedea kwa kuikanda timu ya Simba Sc kwa bao 1-0 wakati wa mchezo wa fainali wa kombe hilo. Mchezo huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya New Amani vilivyopo visiwani Zanzibar na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Hussen Mwinyi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo (kuila) akifuiraha jabo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi, kuila kwake na wadaui wiengne wakati wakitazama mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi Cup kati ya Timu ya Simba SC na Mlandege FC mchezo uliyofanyika visiwani Zanzibar viwanja vya New Amaani

Baadhi ya Maofisa wa Tanzania Commercial Bank TCB wakiwa na watazamaji wengine visiwani Zanzibar katika kufuatilia mchezo wa fainali wa kombe la Mapinduzi Cup yanayofanyika visiwani vya New Amaani Zanzibar


Tanzania Commercial Bank PLC (TCB) ambae ni Moja ya wadhamini wa mashindano ya ligi ya Mapinduzi Cup yanayofanyika visiwani Zanzibar kila mwaka jumamosi iliyopita iyopita Benki hiyo ilikabidhi zawadi ya pesa kiasi cha shilingi milioni Moja kwa golikila bora wa ligi hiyo Athuman Hassan kutoka klabu ya Mlandege Fc Makabidhiano ya zawadi hiyo yalifanyika muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali baina ya Mlandege Fc na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa New Amani Visiwani Zanzibar ambapo mchezo ulikamilika kwa timu ya Mlandege kuibuka na ushindi wa Goli 1-0.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank TCB Adam Mihayo amesema TCB itaendelea kutoa hamasa kwenye michezo mbalimbali hapa Nchini kwani michezo imekuwa ikiwakutanisha watu karibu pia michezo ni ajira.


“Zawadi hii tunazitoa kwa kuleta hamasa kwa wachezaji ili wafanye vizuri na kujitangaza kimataifa ,pia kusaidia kuboresha mchezo huu mwanzo tu Kwa Tanzania Commercial Bank kushiriki katika michezo wa soka hapa nchini”amesema Mihayo.


Tanzania Commercial Bank tumekuwa na utaratibu wakujitolea sana katika jamii kwakufauata misingi ya Benki yetu tumeweza kusaidia sehemu mbalimbali Tanzania bara pamoja na visiwani katika sekta mbalimbali ikiwepo elimu, Afya, michezo, na Biashara na kutoa elimu ya kifedha.

Hapa visiwani Zanzibar tumeshafanya mambo kadhaa ikiwepo kuwasaidia vikundi vya wanawake wajasiliamali kwa kuwapa vitendea kazi vikiwemo vyerehani na kuwawezesha vikundi vya kinamama wa Jimbo la Paje wanaolima zao la mwani kwa kuwajengea kisima Cha furahia ili kuwarahisishia shughuli zao za kilimo wa zao hilo ”

“ Kwa upande wake Golikila wa Mlandege Athuman Hassan alishukuru kupata zawadi hiyo na kuahidi kuwa atazidi kuongeza bidii kuwa kinara na kusaidia timu yake kupta ushindi wa kila mechi. “Napenda kuwashukuru TCB kwa kunipa zawadi hii kwani itakwenda kuongeza sana hamasa upande wangu na wa wachezaji wote na makocha pia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad