HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 30, 2024

SPORTPESA NA VODACOM WAJA NA MCHONGO MPYA…

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
KAMPUNIya Michezo ya Kubashiri ya Sportpesa na Kampuni ya Mtandao wa Simu ya Vodacom wamekuja na mchongo mpya kupitia huduma zao ambazo zitawawezesha wateja kubashiri michezo mbalimbali ya soka na kujishindia kiasi cha fedha.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Sportpesa, Sabrina Msuya amesema kupitia Supa Jackpot ya Sportpesa, wateja waweza kubashiri na kuwa Mabilionea kupitia mtandao wa Vodacom kupitia huduma ya M-PESA.


Sabrina amesema wateja watapata unafuu wa kubashiri michezo yao Sportpesa kupitia Vodacom na kushinda kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 1 endapo utafanikiwa kushinda michezo yote 17 ya Supa Jackpot au kushinda bonasi endapo mteja atabashiri na kushinda zaidi ya michezo 12 hadi 16 kwenye Jackpot.

Kwa upande wao Vodacom wamesema mteja anaweza kubashiri michezo yake ya Supa Jackpot ya Sportpesa kwa kupiga menu ya *150*00# na kuchagua 4 lipa kwa M-PESA, chagua 8 michezo ya kubashiri na chagua 7 Supa Jackpot.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad