HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 3, 2024

SILINDE AZINDUA USAMBAZAJI WA MBEGU ZA RUZUKU ZA ALIZETI MSIMU WA 2023/24

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde amezindua usambazaji wa mbegu za ruzuku za Alizeti  kwa Wakulima katika msimu wa 2023/24.

Zoezi hilo la uzinduzi huo limefanyika leo January 03, 2024 katika Mkoani Singida.

Wizara ya Kilimo kupitia Wakala wa mbegu ASA inatarajia kusambaza jumla ya Tani 2,045 za mbegu bora zilizothibitishwa ubora ikijumuisha tani 700 za mbegu chotara ambazo zinaingizwa kutoka nje ya nchi pamoja na tani 625.4 ambazo zitapatikana kutoka kwa makampuni binafsi ndani ya Nchi.

Aidha, Usambazaji wa mbegu bora kwa mfumo wa ruzuku umeongeza uzalishaji  wa alizeti nchini ambapo kwa msimu huu wa 2023/24 uzalishaji wa alizeti umefikia tani 1,100,000 ikiwa ni ongezeko kutoka Tani 400,000 zilizovunwa mwaka jana 2022/23.

“serikali inatambua gharama za uzalishaji na usambazaji mbegu na changamoto ya mbegu kuwafikia wakulima kwa wakati hivyo kupitia wakala wa mbegu za kilimo Wizara ya Kilimo inaendelea kuwaondolea changamoto hizo kwa kuwafikishia mbegu kwa wakati kupitia Halmashauri mbalimbali,” alisema Silinde.

Aidha Silinde ametoa rai kwa Wakulima kutumia mbegu bora ili kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la Alizeti.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad