Lengo la kikao ni kujadili ushirikiano kati ya Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania katika sekta ya Maji.
Aidha Katika kikao nimeishukuru serikali ya Marekani kwa ushirikiano inautoa katika sekta ya maji na kuahidi kuendeleza zaidi mashirikiano hayo.
Zaidi nimesisitiza kuwa Sekta ya Maji ni sekta muhimu sana na hivyo uwekezaji kama huu una tija kubwa kwa watanzania.
Naye Ndugu Hart, amesema Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na wizara ya Maji na kwamba Serikali ya Marekani imeiweka Tanzania katika mpango maalumu wa mashirikiano ya sekta ya maji, na kiasi cha dollar million 100 zimewekezwa na kutengwa katika sekta ya maji.





No comments:
Post a Comment