Wakala wa usajili ufilisi na udhamini i (RITA )leo wameshiriki maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyoanza toka 24 -30 Januari katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam na viwanja vya nyerere Square mkoani Dodoma . Wiki ya sheria imezinduliwa rasmi leo ambapo mgeni rasmi katika maadhimisho haya kitaifa mkoani Dodoma alikuwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge duniani Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb).
Katika maadhimisho haya wakala unatoa huduma mbalimbali ikiwa pamoja na elimu kuhusu huduma za Wakala,Ushauri wa kisheria bure elimu juu ya kuandika na kuhifadhi Wosia na Mirathi,Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa pamoja na maelelzo ya kina kwa bodi za wadhamini wa Taasisi nyaraka muhimu zinazohitajika wakati wa kusajili kwa njia ya mtandao na pia namna ya kufanya marejesho ya wadhamini
No comments:
Post a Comment