Waziri, wa Elimu , sayansi na teknolojia Prof . Adolf Mkenda ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kupitia Kampuni Tanzu ya Taasisi hiyo (DIT Company) kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuchochea Maendeleo, kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu kwa lengo la kuchangia maendeleo ya uchumii.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na teknolojia ,Omary Kipanga wakati akisoma Hotuba yake alipo mwakilisha waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia Prof. Adolf Mkenda, katika mahafali ya 17 duru ya tatu ya Taasisi ya Teknolojia Dareslaam (DIT ) Kampas ya Myunga iliyopo Wilayani Momba Mkoa wa Songwe.
Amesema kazi nzuri inayofanywa na Kampuni Tanzu ya DIT ya kuimarisha sayansi , Teknolojia na ubunifu imekuwa na mchango makubwa kwa Taifa kutokana na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa Jamii.
"Ninazo taarifa za Kampasi hii kumtumia mmoja wa wabunifu mahiri hapa mkoani Songwe bwana Adam Kinyekile mwenye karakana yake pale Mpemba Tunduma ambaye ni mmojawapo ya washindi wa MAKISATU ambaye Serikal imemfadhili zaidi ya milion 99 kwa ajili ya kuendeleza ubunifu" amesema Waziri Mkenda.
Kwa upande wake Mbunifu Adam Kinyekile amesema Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kupitia Kampuni yake imemsaidia kwa kiasi kikubwa kutambulika ndani ya nchi na nje ambako anauza bidhaa nyingi za kutatua Changamoto za kilimo ambazo anazibuni yeye mwenyewe.
"Nashukuru serikali kwa kunifadhili milioni 99 kwa ajili ya kuendeleza ubunifu wangu ambao umenisadia kwa kiasi kikubwa kuendelea kubuni bidhaa mbalimbali zinazotatua changamoto za kilimo hasa mashine za kupuchua mahindi na trela za kubebea bidhaa mbalimbali hasa mbao baada ya kuvuna na kusafirisha mbolea kupeleka shambani" amesema Adam.
Aidha, wanafunzi wanaonufaika kwa kiasi kikubwa na Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar-es-salaam wameonyesha bunifu mbalimbali walizobuni ambazo zinalenga kutatua changamoto mbalimbali katika taifa za uagizaji vifaa kutoka nje ya nchi.
Vick Mausa ni mwanafunzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam laam ambaye amefanikiwa kubuni mashine yenye gharama nafuu ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya figo yenye gharama ndogo ambayo itauzwa milioni nne tofauti na mashine zinazoagizwa nje ya nchi ambazo huuzwa kwa kiasi kikubwa zaidi ya milioni 20.
" naishukuru Kampuni imeniwezesha kuweka ububifu wangu kwenye vitendo maana nilikuwa na wazo la kubuni hii mashine hivyo kupitia kampuni nimepata vifaa ambavyo nimevitumia kwenye huu Ugunduzi na utakapo kamilika utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za hospitali zetu kukosa mashine za kuwasaidia wagonjwa wa figo" amesema Vick.
Naye Joshua Macha aambaye pia ni mwanafunzi wa DIT anayesoma mwaka Kwanza fani ya Uhandisi ujenzi ameonyesha mashine ya kutengeneza vifaa mbalimbali vya plastiki ambapo ameeleza kuwa alibuni mashine hiyo ambayo tayari inazalisha vifaa tofautitofauti vikiwemo vifaa vya magari na bajaji baada ya kuona uhitaji mkubwa uliopo.
Thursday, January 11, 2024
Home
Unlabelled
PROF.MKENDA AWAPONGEZA DIT KWA KUENDELEA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA NCHINI.
PROF.MKENDA AWAPONGEZA DIT KWA KUENDELEA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA NCHINI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment