HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 5, 2024

NEMC YAPATA MKURUGENZI MPYA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Immaculate Sware Semesi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu na anachukua nafasi ya Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu unaanza tarehe 05 Januari, 2024.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad