Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi ametembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ambapo amepata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) pamoja na kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Kwa upande wake Bw. Mbilinyi ameipongeza timu ya maonesho ya TCAA kwa kujipanga vyema na kutoa elimu stahiki kwa wananchi na wadau mbalimbali wanaotembelea banda hilo.
Bw. Mbilinyi amemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza Johari katika sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamarat Abeid kuhusu kozi zinazotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo ya kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika Banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akipokea zawadi kutoka kwa Mfanyakazi wa TASAC mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akizungumza na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) alipotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Jamila Mbarouk,
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Teophory Mbilinyi akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Salum Pazzy kuhusu kazi zinazofanywa na na Mamlaka hiyo alopotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment