HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 22, 2024

MIKATABA YA MKOA WA MANYARA NI KAMA NDOA YA KIKATOLOKI, UMEJIFUNGA - RC SENDIGA

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Januari 22, 2024, ameshuhudia hafla ya utiaji wa Saini Mikataba 7 yenye Thamani ya Bilioni 2.3.

Mikatabia hiyo itahusisha ujenzi wa lami, ujenzi wa barabara za changarawe, madaraja na matengenezo maalumu katika mtandao wa barabara zinazohudimiwa na TARURA Mkoani Manyara.

Akizungimza kwenye hafla hiyo RC Sendiga, ametoa maelekezo kwa wakandarasi kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo sawa na vigezo na masharti ya mkataba na kuzingatia ubora.
RC Sendiga, amewataka wakandarasi hao kuwapa kipaumbele cha ajira wazawa wa Mkoa wa Manyara, Vikundi vidogo vidogo vya vijana na wanawake ili waweze kukuza vipato vyao.


Mwisho RC Sendiga, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kuboresha miundombinu ya barabara vijijini ambazo baadhi zimeharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha Mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad