HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 26, 2024

MADAKTARI BINGWA KUTOKA HOSPITALI YA TEMEKE WAFIKIA WAGONJWA 577 BUZA

Madaktari bingwa na bingwa bobezi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH) wamefanikisha kambi ya matibabu na uchunguzi, wakiwahudumia wagonjwa 577 na kufanya aina nne za upasuaji katika Kituo cha Afya Buza.

Kambi hiyo iliyodumu kwa siku tano imejumuisha madaktari bingwa katika fani mbalimbali za afya kama upasuaji, macho, kinywa na meno, mifupa, utengamao, masiko, pua na koo (ENT), watoto, wanawake na uzazi, magonjwa ya ndani, afya ya akili, pamoja na uchangiaji damu wa hiari.Matibabu haya ya kibingwa yamefanyika katika wiki ya kuelekea siku ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Raisi Dr Samia Suluhu Hassan, Raisi wa Jamhuri ya Muungana wa Tanzania.

Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dkt. Husna Msangi, Mratibu wa huduma za tiba, amesema wakati wa kuhitimisha kambi hiyo kuwa kambi hiyo ni njia moja wapo ya kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kutoa huduma za kibingwa na bingwa bobezi kwa wananchi katika vituo vya afya.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa za kambi kama hizo kwani zinawapa nafasi ya kupata huduma za kibingwa kwa gharama zilezile za kituo cha afya na hivyo kupunguza usumbufu wa kufuata huduma hizo katika hospitali ya rufaa.

Dkt. Luti Chuwa, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Buza, ameshukuru Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke kwa ujio wa madaktari bingwa hao na kusema kuwa kambi hiyo imenufaisha wakazi wa kata ya Buza. Pia, amekaribisha tena madaktari bingwa kutoa huduma ili kuboresha afya za wananchi.

Bw. Bakari Mdoe, mmoja wa wagonjwa walionufaika na kambi hiyo, amefurahishwa na ujio wa madaktari bingwa kutoka Temeke na kuwahimiza wananchi kutumia fursa kama hizo kupata matibabu




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad