HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 25, 2024

KAMATI YA PAC YAPOKEA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA KUKUZA UJUZI KWA VIJANA

 

 

 Na, Mwandishi Wetu - DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imepokea taarifa ya Programu ya kukuza Ujuzi wa Nguvu Kazi nchini inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akizungumza leo Januari 24, 2024 baada ya kupitia na kuchambua wasilisho la Ofisi hiyo Fungu 65 kuhusu programu hiyo, amesema wasilisho hilo litasaidia kamati kutoa ushauri utakaoongeza ufanisi kwenye utekelezaji wake wa kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira.

Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema serikali imeendelea kutanua wigo wa ukuzaji ujuzi kwa vijana na hadi sasa wamenufaika 141,968 kupitia programu ya kukuza ujuzi iliyoanza kutekelezwa Mwaka 2016/17.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilishwa na wajumbe wakati wa kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)  cha kutoa taarifa ya Mradi wa Ukuzaji Stadi unaotekelezwa na ofisi hiyo kilichofanyika leo tarehe 24 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ally Msaki akiwasilisha taarifa ya Mradi wa Ukuzaji Stadi unaotekelezwa na ofisi hiyo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha kutoa taarifa ya Mradi huo kilichofanyika leo Januari 24, 2024 Bungeni jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)   wakifuatilia wasilisho la taariya ya Mradi wa Ukuzaji Stadi unaotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu wakati wa kikao cha kamati hiyo cha kupokea taarifa hiyo Kilichofanyika leo tarehe 24 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma.










No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad