HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 24, 2024

IDARA YA FORODHA TRA KUADHIMISHA SIKU YA FORODHA DUNIANI JANUARI 26

Kaimu Kamishna wa Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Hassan Juma akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Januari 24, 2024, wakati wa Kutambulisha Maadhimisho yatafanyika jijini Dar es Salaam yakiambatana na kuwatambua baadhi ya Wadau wa Forodha.


Na Avila Kakingo Michuzi Tv
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Forodhainatarajia kuadhimisha Siku ya Forodha Duniani Januari 26, 2024 ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe hiyo na mwezi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Januari 24, 2024, Kaimu Kamishna wa Forodha, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Hassan Juma amesema Maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam wakiambatanisha na kuwatambua baadhi ya wadau wa Forodha.

"Inapofika Januari 26 kila mwaka Idara ya forodha Tanzania kama mwanachama wa Mamlaka ya Forodha Duniani huwa inaadhimisha siku ya Forodha."

Siku ya maadhimisho hayo yanalengo la kufikisha ujumbe kwa Umma juu ya shughuli zinazofanywa na Wadau wa Forodha nchini lakini pia kutambua wadau ambao wanashirikiana nao katika kufanya shughuli za forodha.

Kwa mwaka huu Mamlaka ya Forodha Ulimwenguni (WCO), imetoa kauli mbiu ya Kutambua na Kuthamini juhudi na michango ya wadau mbalimbalimba wanaoshirikiana na Wakala wa forodha katika kutimiza majukumu ya kiforodha.

Amesema kuwa watawatambua wadau wa Forodha ambao wanafanyanao kazi ambao wanaweza kuwa Serikali, Makampuni binafsi na Umma unaoishi maeneo hayo ambao wanasaidia kutekeleza majukumu ya Kiforodha ambayo ni Kukusanya Mapato, Kusimamia mipaka na kuilinda jamii.

Amesema utambuzi huo unatokana na majukumu ya kukagua bidhaa zinapoingia nchini ambazo haziruhusiwi lakini pia bidhaa zinazoingia nchini mpaka kupata vibali au ruhusa.

Akizungumzia majukumu mojawapo ya Mamlaka ya Forodha hapa nchini na ulimwenguni kote ni kusimamia, kukusanya mapato ya Serikali na kulinda jamii ya watumiaji wa bidhaa mbalimbali.

Pia wanajukumu la kusimamia mipaka yote ambayo watu na bidhaa zinaruhusiwa kuingia au kutoka nchini na kutoa takwimu sahihi za bidhaa zinazoingia nchini.

"Idara ya Wakala wa Forodha inakusanya karibia asilimia 40 ya Mapato yote yanayokusanywa na TRA." Amesema

Akizungumzia namna teknolojia ilivyoweza kusaidia Kaimu Kamisha wa Forodha Hassan amesema kuwa zamani walikuwa wakiwasilisha nyaraka kwa mkono kwa sasa hicho kitu ni historia kwasasa ni zinatumwa kwa mtandao, ambapo unapata tathmini ya kila kitu hapo hapo pamoja na Kulipia.

Pia ukaguzi wa Mizigo amesema kuwa wanatumia kifaa maalumu cha ukaguzi ambacho hufanya kazi kwa muda mfupi zaidi ambapo zamani ilichukua muda mwingi na rasilimali watu wengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad