HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 10, 2024

WANAFUNZI WA LEO NDIYO VIONGOZI WA BAADAE -DC LUDIGIJA

 

 


Akizungumza na walimu na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamilama Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza,Ng' wilabuzu Ludigija amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa sana kwa kuweka mazingira wezeshi na rafiki katika upatikanaji wa elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa ya kisasa.

Amewaomba wazazi na walezi kuunga mkono maendeleo hayo wananchi hawana budi kuwaruhusu watoto kuripoti shuleni na kuanza masomo mara moja ili kutengeneza kizazi cha uelewa kwani wanafunzi wa leo ndiyo viongozi wa baadaye.



Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza Ng' wilabuzu Ludigija amefanya ziara  kutembelea shule ya Sekondari Nyamilama iliyopo Halmashauri ya Kwimba Mkoani Mwanza na kujionea Wanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa masomo wakiwa wameripoti vizuri  katika shule za serikali.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyamilama  wakia darasani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad