HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 9, 2023

Sekta ya Usafirishaji ndio msingi wa maendeleo nchini

 


WAKATI Sekta ya usafirishaji ikitajwa kuwa ndio msingi wa maendeleo endelevu wahitimu wa mafunzo ya umahili katika Chuo cha Taifa cha Usafirishahi (NIT) wamekumbushwa kuhakikisha sekta hiyo inawanufaisha wananchi...

Hayo yamesemwa Desemba 2023, na Giliard Ngewe Mkurugenzi mtendaji Udart wakati wa utoaji wa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri kwenye vitivo mbalimbali vya chuo hicho.

"Leo ni siku ya Convocation kwa wahitimu wa NIT wamepewa zawadi ili wapate motisha wakatoe huduma za usafirishaji itakayowanufaisha Watanzania wote" alisema.

Amewasisitiza wahitimu hao wakafuate sharia ili abiria na vyombo viwe salama.

Amesema kuwa mchango wa NIT kwenye sekta hiyo ni mkubwa na kwamba unalisaidia taifa.

Naye Zainabu Mshana Kaimu Mkuu wa Chuo hicho amesema kuwa Chuo hicho kinajivunia kutoa wataalam wanaokwenda kutoa suluhisho la usafiri nchini.

"Mwaka jana walihitimu wanafunzi 2700 lakini mwaka huu wamehitimu wanafunzi 3600 tunajuvunia kutoa wataalam waliopata mafunzo ya umahili kwa lengo kutatua changamoto za usafiri" alisema.

Amesema kuwa wanafunzi hao watakuwa chachu ya maendeleo kwa kuwa sekta hiyo ndio msingi wa maendeleo.

"Kupitia ujuzi wao watatuletea maendeleo endelevu kwa kuwa usafirishaji ndio msingi wa maendeleo" alisema.

Bariki Seme Mhitimu wa Stashahada katika ukarabati wa Meli amesema kuwa amefurahi kuhitimu mafunzo hayo na kwa kuwa nchi ina malengo ya kujikita kwenye uchumi wa Bluu basi basi atatoa mchango wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad