HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 15, 2023

BILIONI 8 ZA SAMIA ZAONGEZA USTAWI KWA WENYE ULEMAVU – KATAMBI

 

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ametoa zaidi ya Bilioni 8 kwa ajili ya ustawi wa Watu wenye Ulemavu.Hayo yamebainisha Desemba 14, 2023 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Ofisi hiyo.

Amesema Serikali imetoa kiasi cha shilingi 3.46 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa Vyuo vya Ufundi stadi na marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vilivypo  Saba Saba, Yombom, Mtapika, Masasi na Luanzari

“Serikali imeendelea kutoa mafunzo kupitia  vyuo 6 vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu ambavyo ni Sabasaba, Yombo, Luanzari, Masiwani, Mtapika, Masasi ambapo  kiasi cha shilingi 568 Milioni kimetumika kuwezesha mafunzo husika” amesema.

Amesema Serikali inaendelea na  ujenzi wa Vyuo vipya vinne vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vya Songwe, Mwanza, Kigoma na Ruvuma ambapo kiasi cha Shilingi Bilion 3.4 kimetumika na kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kiasi cha shilingi 3 Bilioni kimetengwa kwa ajili kuendeleza ujenzi kwa Vyuo.

Aidha, Mhe. Katambi amesema Serikali ilitoa kiasi cha million 960 kwa ajili ya Ujenzi wa mabweni katika shule zenye watoto wenye mahitaji maalum na ilitoa  shilingi 62 milioni kwa ajili ya ununuzi wa maligafi za utengenezaji wa mafuta ya ngozi ya Watu wenye Ualbino.

Sambamba na hayo, amesema Serikali imetoa kiasi cha shilingi 4.26 Bilion kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya usikivu kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum na vifaa husika vimesha nunuliwa na kusambazwa.

Awali akizungumzia usimamizi wa kazi na huduma za ukaguzi, amesema Serikali imechukua hatua kwa waajiri wanaothibitika kukiuka Sheria za Kazi ambapo jumla ya Waajiri 199 wamepatiwa amri tekelezi kutakiwa kurekebisha mapungufu ya kisheria yaliyobainika na waajiri 2 wamefikishwa Mahakamani.

“Mwaka 2021/2022 jumla ya  shilingi bilioni 1.8 zilitolewa kwa vijana kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali, Julai hadi Desemba, 2023 jumla ya shilingi 1,274,471,500  zimetolewa kwa miradi  ya vijana 56 yenye vijana 392 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya vijana (YDF). amesema.

Kwa upande wa vijana, Mhe. Katambi amesema shilingi  2,700,000,000 zimetumika Kukamilisha maandalizi ya Vijana 6,000 watakaoanza mafunzo ya uanagenzi awamu ya sita katika vyuo 42 nchini. 

Sambamba na hayo, amebainisha suala la huduma za ajira nchini ambapo amesema hati za Makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya kazi na ajira kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi mbili za kimkakati zimesainiwa,  sawa na asilimia 100 ya lengo la kusaini na nchi 2 kwa mwaka.







 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad