Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa vyama vya siasa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na viongozi wanawake wa vyama siasa nchini mara baada kifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa vyama vya siasa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja viongozi wa vyama vya siasa mara baada kifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa vyama vya siasa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
*Wanasiasa waaswa kupeleka elimu ya matokeo ya sensa kwenye majukwaa yao.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 imekuwa tofauti katika miaka yote kuweka majengo na anuani hali ambayo imeweza kurahisisha biashara Mtandao na serikali kupata mapato yake
Profesa Ndalichako ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Uwasilishaji ,Usambazaji,Uhamasishaji wa Matumizi ya Sensa na Makazi ya Mwaka 2022 kwa viongozi wa vyama Siasa iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa mafunzo kwa viongozi wa vyama siasa wana umuhimu katika katika kupanga mipango ya maendeleo kwenye jamii.
Amesema kuwa mtu akifanya biashara ya kwa kutumia mtandao mteja anafikiwa kirahisi na kuokoa muda wa kuuliza.
Amesema kuwa kwa kutumia matokeo ya sensa yanakwenda kutatua changamoto mbalimbali
Profesa Ndalichako amesema ushiriki wa vyama vya siasa umekuwa na mchango mkubwa wa kufanikisha kufanya sensa na kupata matokeo.
Amesema katika sensa vyama viliungana bila kujali itikadi zao kwa kujua jambo linalifanyika ni kwa masilahi mpana ya taifa katika kupanga maendeleo ya wananchi.
Hata hivyo amesema wanasiasa ni kiungo muhimu katika kufikisha matokeo ya sensa katika kupanga mipango na kuwa kwenye mijadala ya namna ya kutumia matokeo hayo kw kutoa maoni katika miradi mbalimbali kutokana na mahitaji yao.
Amesema kuwa Sensa ya mwaka 2022 yatawezeha kufikia dira ya malengo ya miaka 50 ijayo.
Profesa Ndalichako amesema matokeo hayo ya sensa yataongeza uwajibikaji pamoja na kuhimiza wananchi katika shughuli za kiuchumi.
Amesema mafunzo hayo wanayoyatoa kwa Makundi mbalimbali yamekuwa na msaada mkubwa kwa watu kwani wamekuwa wakielimisha juu ya uwepo wa ramani ya maeneo yao na kuonyesha kila kitu ambapo inasaidia sasa wananchi kuwajibika kimaendeleo katika maeneo yao.
"Sensa ya mwaka 2022 imemalizika,Sasa nchi inajiandaa na nyingine ambapo hii inatusaidia kuonyesha kwa uhalisia maeneo gani ambayo hayajapata kipaumbele katika maendeleo kwani kuna baadhi ya vijiji viliomba kujengewa shule lakini unakuta watoto ni wachache ,unakuta Kiongozi mmoja alikuwa na sauti hivyo Kila kitu kinaenda kwake,"amesema na kuongeza.
"Hivyo sasa maeneo ambayo hayajapata kipaumbele ndo yatapewa kipaumbele na hapo tutauliza sensa inasemaje katika kupeleka Maendeleo katika eneo hilo,"amesema.
Kamisaa wa Sensa Zanzibar Balozi Mohamed Haji Hamza amesema kuwa viongozi wa siasa walikuwa mstari mbele hakuna hata mtu mmoja aliyetaka watu wasijitokeza kuhesabiwa.
Kamisaa Hamza amesema Sensa iliyofanywa na kuja na matokeo ambayo yanakwenda kurahisha katika upangaji wa rasilimali kwenda katika maeneo husika maeneo yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Kaimu Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu wa NBS Ruth Minja amesema katika matokeo hayo NBS imekuwa ikielemisha makundi mbalimbali.
Amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa mujibu wa mwongozo wa kitaifa wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
"Mwongozo huo umeeleza mafunzo haya yafanyike kuanzia ngazi ya taifa hadi ya chini kabisa za utawala kwa makundi mbalimbali, " amesema Minja.
No comments:
Post a Comment