HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 11, 2023

PBPA :Serikali kujenga miundombinu mikubwa ya uhifadhi mafuta.

 

Mifumo ya Uagizaji wa Mafuta nchini waokoa Bilioni 500

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
 
Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka mitatu kupitia Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wamedhamiria kujenga miundombinu ya kupokea meli za mafuta Tani za kutosha kwa wakati moja.

Hayo ameyasema Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Erasto Simon wakati akizungumza na wahariri chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kujenga miundombinu hiyo itasaidia kupunguza idadi ya meli kushusha mafuta ambapo ucheleweshaji ushushaji ndio unafanya kuwa na meli nyingi za mafuta kutokana na uwezo wa uhifadhi wa mafuta hayo.

Simon amesema kuwa kutokana na uagizaji wa mafuta kutumia ya Dola ya Marekani sasa serikali imeweka utararibu wa kuweza kutumia fedha za nchi nyingine katika kuhakikisha wanaondoa changamoto ya kupungua kwa dola nchini.

Kaimu Mtendaji Mkuu U wa PBPA amesema kuI kuwa Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imekuwa ikitoa kiasi cha fedha cha Dola za Marekani kwa Benki za Biashara ili ziweze kulipia mafuta yanayotumika nchini hayo ni maono ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan 


Aidha amesema kupanda kwa mafuta kuna changamoto ikiwemo kwa vita ya Urusi na Ukraine na wakati wa UVIKO  19 mafuta yalishuka lakini ikaja kupanda kutokana na usafirishaji.

Simon amesema katika historia hadi kuanzishwa kwa wakala nchi imepita mabonde na milima lakini sasa baadhi ya nchi zinajifunza Tanzania katika uagizaji wa mafuta.

Amesema kutokana na mifumo waliyoiweka Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA) inajua  kodi  ya mafuta pale tu meli inapoanza safari.


Hata hivyo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeokoa zaidi ya Shillingi Bilioni 500 kutokana na uwepo wa mfumo wa uagizaji Mafuta kwa pamoja.

Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nishati ya mafuta inapatikana wakati wote na kwa bei nafuu kutokana na mifumo iliyowekwa.

“ Serikali ya Awamu ya Sita imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa ruzuku kwenye gharama ya mafuta kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai, 2022 hadi Disemba, 2022  kupunguza bei ya mafuta kwa wananchi na kuwa bei  stahimilivu kwa mlaji wa mwisho , amesema Kaimu Mtendaji Mkuu wa PBPA  Simon.

Simon amesema  Serikali kupitia Benki Kuu ilibadilisha baadhi ya miongozo ya udhibiti wa Dola za Marekani ili kuwezesha Benki za Biashara kupata fedha hizo kutoka sokoni.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) Erasto Simon akizungumza na Jukwaa la  Wahariri  Tanzania (TEF) na Waandishi wa Habari kuhusiana na mafanikio ya PBPA  kwa miaka mitatu  ya  Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Jijini Dar es Salaam
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza kuhusiana na uratibu wa Ofisi hiyo kwa Taasisi zilizo chini ya Msajili kueleza juu ya ufanisi wa kazi zao ,jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari katika mkutano kati ya TEF na OSHA jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad