HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 21, 2023

NBAA YATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI YA MWEZI NOVEMBA 2023, YAZINDUA MTAALA MPYA WA MASOMO YA BODI


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imetangaza matokeo ya mitihani ya 98 iliyofanyika mwezi Novemba mwaka 2023 ya Bodi ambapo takwimu zinaonesha watahiniwa 6711 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ufaulu ni asilimia 66.6

Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema Ufaulu umepungua kutoka asilimia 67 mpaka 66.6 ambapo watahaniwa 527 hawakuweza kufanya mitihani kwa sababu mbalimbali, hivyo idadi ya watahaniwa 6711 sawa na asilimia 92.7 walifanya mitihani ambapo wanawake walikuwa 3636 sawa na asilimia 50.2 na wanaume 3602 sawa na asilimia 48.8

Pia Bodi hiyo imezindua mihutasari mipya pamoja na vitabu vya rejea ambapo Bodi ya NBAA hufanya mapitio ya mtaala yake pamoja na vitabu kila baada ya miaka mitano.

Maneno amesema Bodi ilianza mchakato wa kupitia mitaala yake pamoja na vitabu rejea kuanzia mwezi Agosti mwaka 2022 na zoezi hili lilianza kwa kufanya marekebisho ya Mtaala na  baadae zoezi la kupitia vitabu rejea lilifanyika.

"Bodi inaendelea kuboresha mitaala ya kufundishia ili kuongeza idadi ya Wahasibu na Wakaguzi hapa nchini ili kuweza kuchangia katika maendeleo hasa kuhakikisha Hesabu tunazozitoa zinakuwa ni sahihi na zinaaminika." akisema Maneno

Pia CPA MAneno  amesema Bodi itaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali za elimu ili kuhakikisha  maadili yanazingatiwa ili vijana waandaliwe tangu wakiwa vyuoni .
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akizindua mitaala mipya ya masomo ya Bodi itakayoanza kutumika Januari mwaka 2024 na kuanza kufanyiwa Mitihani Novemba mwaka 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akionesha mitaala mipya ya masomo ya Bodi kwa waandishi wa Habari mara baada ya kuzindia mitaala hiyo iliyofanyika katika ofisi za Bodi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akizundua vitabu vya rejea vitakavyoanza kutumika kuanzia mwaka 2024  wakati wa mkutano na waandishi wa habari waliofika ili kupata taarifa mbalimbali za Bodi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akionesha vitabu rejea pamoja na Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo, Peter Lyimo(wa kwanza kushoto) na Mkufunzi CPA Rashid Mganwa(wa kwanza kulia) wakati wa kutangaza matokeo pamoja na kuzindua mitaala mipya wa masomo itakayoanza kutumika mwaka 2024.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutangaza matokeo ya mitihani ya 98 ya Bodi, uzinduzi wa Mitaala mipya ya Bodi pamoja na Vitabu rejea  pamoja na sheria ndogo za mafunzo ya Mitihani ya Wahasibi na Wakaguzi ya Mwaka 2023.
Mkutano ukiendelea 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad